Germany Win Under-19 European Championships
Tibor Illyes/Associated Press
Kweli hiki ni kiangazi cha soka la ujerumani,
Timu ya ujerumani ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 19 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ulaya, chini ya miaka 19 baad ya kuifunga Ureno kwa bao 1-0 huko Budapest.
Goli pekee la washindi limefungwa na Hany Mukhtar.
 
engine hiyo ni dalili ya kuwa Ujerumani itabaki kuwa tishio kwa miongo kadhaa kwani soka lao wameliandaa na wamepanga nani atakuwa mrithi wa wakongwe wa sasa.



Na Boniface Wambura, Johannesburg
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama juzi (Julai 30 mwaka huu) hapa Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo- asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.
Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia wachezaji.
Serengeti Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).


SIMBA IMEENDELEA NA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI KUU BARA IKIWA CHINI YA ZDRAVKO LOGARUSIC PAMOJA NA MSAIDIZI WAKE SELEMANI MATOLA. MAZOEZI HAYO YALIFANYIKA KATIKA ENEO LA BUNJU, NJE KIDOGO YA JIJI LA DAR ES SALAAM.







 
Credits:Saleh Jembe Blog.
Inter Milan vs. Manchester United: Score, Grades, Reaction for Pre-Season Match
KOCHA Louis van Gaal ameendeleza wimbi la ushindi baada ya Manchester United kuifunga kwa penalti 5-3 Inter Milan kufuatia safe ya 0-0 katika mchezo wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa FedEx Field mjini Washington, penalti za United zilitiwa nyavuni na Ashley Young, Javier Hernandez, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Darren Fletcher wakati Marco Andreolli wa Inter aligongesha mwamba. Van Gaal akipanga vikosi viwili, kimoja kila kipindi.
Man United kipindi cha kwanza: Lindegaard, Smalling, Jones, Evans, Valencia, Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney, Welbeck
Kipindi cha pili: De Gea; M Keane, Evans, Blackett; Young, Cleverley, Fletcher, Kagawa, Shaw; Zaha, Nani/Hernandez dk77.
Inter Milan: Handanovic/Carrizo dk63, Ranocchia, Vidic/Andreolli dk72, Juan Jesus, D'Ambrosio, Jonathan, Kuzmanovic/Laxalt dk63, Krhin/M'Vila dk46, Dodo/Nagatomo dk63, Botta/Taider dk63 na Icardi.

Mwanzo mzuri: Shinji Kagawa, Darren Fletcher na Tom Cleverley, wachezaji watatu waliofunga penalti za United wakishangilia baada ya ushindi wa 5-3 dhidi ya Inter Milan
Happy: Louis van Gaal and Ryan Giggs smile after the success
Kocha Louis van Gaal na Msaidizi wake, Ryan Giggs wakifuarahia
 
Credits: Bongostaz.com
 
AZAM FC imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, maarufu kama Rollingston baada ya kuichapa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ya Mgulani Twalipo bao 2-0 katika fainali jioni hii Uwanja wa karume, Dar es Salaam. Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ aliyefunga bao la kwanza dakika ya tatu, baada ya kuwatoka vizuri beki wa kulia wa Twalipo, Ally Mbonde na beki wa kati Ally Athumani kisha kumtungua kipa wao, Kulwa Baumba.
 
Huku Adam Omar Soba akiifungia Azam FC bao la pili dakika ya 88 na kuihakikishia ushindi wake.
Mabingwa; Wachezaji wa Azam FC wakisherehekea na Kombe lao la ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, maarufu kama Kombe la Rollingston walilokabidhiwa baada ya kufunga Twalipo mabao 2-0 katika fainali Uwanja wa Karume, Dar es Salaam hapo jana.






Roma vs. Manchester United: International Champions Cup Score, Grades, ReactionWayne Rooney ameng'ara katika mechi ya Man. United dhidi ya AS Roma akiisaidia timu yake kufunga magoli mawili kati ya matatu dhidi ya AS Roma.
Rooneyalifunga goli la kwanza dakika ya 36 akifunga kwa shuti la umbali wa yadi 22 na kumuacha kipa wa As Roma hana la kufanya,

Goli la Kwanza:

dakika tatu baadaye Roooney tena alikuwa msaada mkubwa kupitia pasi aliyoitooa kwa Juan Mata ambaye alimalizia na kuandika goli la pili.Roone alifunga tena goli a tatu katika dakika ya 47 ya nyongeza kipindi cha kwanza baada ya Danny Welbeck kuangushwa eneo la hatari.

Goli la Pili:
 

La tatu:
 
As Roma walipata magoli yao dakika ya 76 kupitia kwa Miralem Pjanic na Dak.ya 89 likifungwa na kwa  mkongwe Francesco Totti. 

Ushindi huo unakuwa ushindi wa pili kwa kocha Van Gaal baada ya ule wa 7-0 dhidi ya Galaxy,ambaye kuingia kwake Man. U kumeonesha kuleta uhai na kuamsha ari ya wachezaji.

Neymar ametua jijini Barcelona, Hispania lakini hataanza kazi na kikosi cha Barcelona.
Badala yake atakwenda kujichimbia Ibiza na kuendelea kula raha huku akiendelea na matibabu.
Daktari ameeleza, Neymar amekuwa akipata nafuu haraka kuliko ilivyotegemewa kutokana na maumivu makali baada ya kuvunjika sehemu ya uti wake wa mgongo.
Neymar aliumizwa na beki wa Colombia, Juan Zuniga wakati wa michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika hivi karibuni.
Akiongizana na mpenzi wake, Bruna Marquezine, Neymar alitua Barcelona na mara moja ameondoka kwenda Ibiza.



MWANA FA




Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, mapema wiki hii alijikuta akijibizana hoja na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ juu ya mwelekeo wa timu ya taifa, Taifa Stars, mara baada ya matokeo ya mabao 2-2 dhidi ya Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili iliyopita.



Mwana FA ambaye ni mdau mkubwa wa soka, alitoa hoja kwa Malinzi katika mtandao wa Twitter, ambapo alilalamika juu ya mahudhurio hafifu ya mashabiki katika mechi, ambapo ilielezwa yalitokana na ukubwa wa kiingilio kilichopangwa na TFF, lakini Malinzi alipinga hoja hiyo.



Sehemu ya majibizano yao ilikuwa hivi:
Mwana FA: Mheshimiwa Jamal Malinzi, nadhani hii kauli inatufaa na sisi...mahudhurio hafifu yanashusha morali za wachezaji wetu.

Malinzi: Mwana FA timu yoyote isiposhinda visingizio huwa havikosekani, Tanzania vs Zimbabwe waliingia watu 8,000 tu na tukashinda, juzi waliingia 20,000 tukapata sare.

Mwana FA: Jamal Malinzi siyo lazima kushinda kila siku, kama mwanamichezo naelewa, ni kuhusu kutengeneza mazingira 'yanayowabeba' wapenzi na wachezaji wetu.

Baada ya hapo, Malinzi hakutaka tena kuendelea na mjadala huo licha ya wadau wengine kuendelea kutoa maoni mtandaoni hapo, ambapo wengi wao walionekana kuitupia lawama TFF kutokana na kuweka kiingili cha chini kuwa shilingi 7,000 ambacho walikilalamikia kuwa ni kikubwa.



Leader: Mourinho (right) struck up a brilliant relationship with the Chelsea legend
Didier Drogba anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja katika klabu yake ya zamani ya Chelsea wiki ijayo sasa akirudi kama mchezaji na kocha.

Mchezaji huyo ambaye alipoingia Chelsea kwa mara ya kwanza alipewa mkataba wa miaka 10, amekuwa huru baada ya kuiacha Galatasaray.
Kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa  L'Equipe Mourhino ndiye aliyemshawishi Drogba kurudi Stamford Bridge.
Drogba aliondoka Chelsea mwaka 2012 baada ya kuiongoza kupata taji la Kwanza la mabingwa wa ulaya akifunga goli la ushindi dhidi ya Bayern katika fainali iliyochezwa nchini Ujerumani.
 Mourhino tayari pia amemleta mshambuliaji Diego Costa kwa kitita cha Euro 32 mil. kutoka Atletico, kufuatia kuondoka kwa Samuel Eto'o na Demba Ba, walioelekea Besikitas. 







Mafataki.



Malkia akifungua rasmi.






   
 Z Pellets WAC 1-1 Chelsea
Wakati Chelsea inatoka Sare 1-1 kwenye Mechi ya Kirafiki na RZ Pellets huko Austria hapo Jana, Meneja wao José Mourinho amesema yupo tayari kumhuzunisha mmoja wa Makipa wao.
Petr Cech Jana alicheza baada ya kuwa nje kwa muda mrefu alipoumia Msimu uliopita
lakini Chelsea wanakaribia kumkaribisha Kipa Thibaut Courtois aliekuwa huko Atletico Madrid kwa Mkopo kwa Misimu Mitatu.
Cech aliumia Mwezi Aprili kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Chelsea
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
16 Julai Wycombe Wanderers 0 Chelsea 5 (Magoli: Bamford, Brown 2, Terry, Ivanovic)
19 Julai AFC Wimbledon 2 Chelsea 3, Kingsmeadow
23 Julai RZ Pellets WAC 1 Chelsea 1, Klagenfurt, Austria
27 Julai NK Olimpika Ljubljana v Chelsea, Ljubljana, Slovenia
30 Julai Vitesse Arnhem v Chelsea, Arnhem Stadium, Netherlands
3 Agosti Werder Bremen v Chelsea, Wesser Stadium, Germany
10 Agosti Ferencvaros v Chelsea, Albert Florian Stadium, Budapest, Hungary
12 Agosti Chelsea v Real Sociedad
+++++++++++++++++++++++++++
Sporting Kansas City 1 Man City 4
Manchester City wameinyuka Sporting Kansas City Bao 4-1 kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa huko Kansas, USA Alfajiri hii.
Bao za City zilifungwa na Bruno Zuculini Dakika ya 3, Dedryck Boyata, 45, Kolarov, 72 na Iheanacho, 88.
Bao pekee la Kansas City C.J Sapong kwenye Dakika ya 30.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 1-1.
Man City
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
13 Julai Dundee 2-0 Man City
18 Julai Heart of Midlothian 1-2 Man City (Sinclair, Kolarov)
23 Julai Sporting Kansas 1 Man City 4, Kansas, USA
Guinness International Champions Cup
27 Julai
AC Milan v Man City, Heinz Field, USA
30 Julai Liverpool v Man City, New York, USA
2 Agosti Olympiacos v Man City, Bank Stadium, USA
Ngao ya Jamii
10 Agosti Man City v Arsenal, 17.00, Wembley Stadium
LIVERPOOL 0 AS ROMA 1
Bao la kujifunga mwenyewe la Daniel Agger limewapa ushindi AS Roma wa Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa huko Fenway Park Alfajiri hii.
Kila Meneja, Brendan Rodgers wa Liverpool na Rudi Garcia wa AS Roma, alishusha Kikosi kikali.
Lakini ni AS Roma ndio waliibuka kidedea kwa Bao la Dakika ya 90.
VIKOSI:
Liverpool: Jones, Kelly, Skrtel, Coates, Enrique, Lucas, Allen, Coutinho, Borini, Lambert, Ibe
AS Roma: Skorupski, Somma, Benatia, Castan, Cole, Florenzi, Keita, Nainggolan, Iturbe, Totti, Ljajic.
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
16 Julai Brondby 2-1 Liverpool (Peterson)
19 Julai Preston North End 1 Liverpool 2, Deepdale
23 Julai AS Roma 1 Liverpool 0, Boston, USA
Guinness International Champions Cup
27 Julai Olympiacos v Liverpool, Chicago, USA
30 Julai Manchester City v Liverpoo, New York, USA
2 Agosti AC Milan v Liverpool, Charlotte, USA
10 Agosti: Liverpool v Borussia Dortmund, Anfield
+++++++++++++++++++++++++++




Kikosi cha Taifa Stars kimerejea jijini Dar es Salaam leo kutoka Mbeya ambapo Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kitapambana na Msumbiji (Mambas) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Benchi la Ufundi la Taifa Stars pamoja na wachezaji kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga Seaview jijini Dar es Salaam.

Naye mchezaji Mwinyi Kazimoto amewasili leo 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways kutoka Qatar ambapo anacheza mpira wa miguu katika klabu ya Al Markhiya ya huko. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi katika hoteli ya Protea Courtyard.




 Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwakabidhi vifaa Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Yanga George Simba 

Ikiwa ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya msimu wa 2014/15 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema “Tunawapatia vifaa mapema kabla ya ligi kuanza ili wapate muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2014/15 ambayo bila shaka itakuwa na changamoto kubwa kwa timu hizi mbili na pia tunaamini kuwa siri ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri. Ni matumaini yetu kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa Simba na Yanga wataiwakilisha Kili vizuri na kufurahia kuzichezea klabu hizi kongwe.”


Kavishe aliongeza kuwa Vifaa ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi, shin guards, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu.

Kilimanjaro Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.  


Kavishe alisema kuwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga umelenga kukuza soka la Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa.

Tunawashukuru viongozi wa Simba na Yanga, mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu.

“Tunawaomba mashabiki wa Simba na Yanga waendelee kuiunga mkono bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager kwani tunafanya kila jitihada kuwapa burudani na kufikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.”
 
HIKI NDICHO KINATARAJIWA KUWA KIKOSI KIPYA CHA REAL MADRID BAADA YA UGENI WA WACHEZAJI NYOTA KAMA KROOS, FALCAO NA JAMES RODRIGUEZ AMBAO WANATARAJIWA KUTUA HIVI KARIBUNI. JAMAA WATATISHA.
BRONDBYvLIVERPOOL


Liverpool Leo hi huko Brondby, Denmark walichapwa Bao 2-1 katika Mechi yao ya kwanza ya Ziara yao ya kabla Msimu mpya kuanza walipofungwa na Wenyeji wao Club Brondby IF.
Wakiwa chini ya Meneja wao Brendan Rodgers ambae Msimu uliopita alifanya kazi kubwa kuisaidia kumaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Manchester City, Liverpool walichezesha Kikosi mchanganyiko na Kipindi cha Pili kilipoanza kubadili Wachezaji kumi.
Bao la kwanza la Brondby lilifungwa na Christian Norgaard kwenye Dakika ya 24.
Hadi Mapumziko Brondby 1 Liverpool 0.
Liverpool walisawazisha katika Dakika ya 48 kwa Bao la Kristoffer Peterson ambae aliingizwa kutoka Benchi.
Bao la ushindi kwa Brondby lilifungwa na Mchezaji wao kutoka Macedonia, Ferhan Hasani katika Dakika ya 90.
Hadi mwisho, Brondby 2 Liverpool 1.
Mechi inayofuata kwa Liverpool ni dhidi ya Preston Northend hapo Julai 19.
KIKOSI:
Liverpool:
Brad Jones, Kelly, Agger, Ilori, Smith, Lucas, Rossiter, Coutinho, Suso, Borini, Teixeira
Akiba: Ward, Allen, Ibe, Coady, Skrtel, Flanagan, Phillips, Wisdom, L. Jones, Peterson, Stewart
LIVERPOOL-ZIARA KABLA MSIMU:
16 Julai Brondby 2 Liverpool 1[Brondby, Denmark]
19 Julai Preston North End v Liverpool [Deepdale, Preston]
24 Julai Roma v Liverpool [Boston, USA]
28 Julai Liverpool v Club Olympiakos Nicosia


Karibu ulete mataji: Kocha mpya wa Manchester United,
Louis Van Gaal kushoto akikaribishwa katika ofisi yake mpya na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward makao makuu ya Mashetani hao Wekundu, Carrington

Van Gaal akiwa na Kocha Msaidizi, Ryan Giggs kushoto

Aliwasili na ndege hii binafsi Uwanja wa Ndege wa Manchester leo asubuhi
Baada ya safari ndefu ya Mwezi mzima iliyoanzia Juni 12, hapo Jumapili Fainali za Kombe la Dunia Nchini Brazil zitafikia tamati huko Estadio Maracana, Jijini Rio de Janeiro Nchini Brazil, kwa Mechi ya Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Germany na Argentina.
Huu ni Mtanange kati ya La Albiceleste, kama inavyoitwa Argentina ikimaanisha Nyeupe na Bluu, Rangi ya Bendera ya Nchi yao, dhidi ya Die Mannschaft, ikimaanisha Timu kama inavyoitwa Germany.
Germany imetinga Fainali hii kwa kishindo kikubwa kilichotikisa Dunia baada ya kuwabwaga Wenyeji wa Mashindano Brazil Jumanne iliyopita kwa kipondo cha Bao 7-1 huku wakifunga Bao zao 5 za kwanza ndani ya Dakika 29 na Bao lao la Pili hadi la 5 yakipigwa ndani ya kipindi cha Dakika 6 tu.
Argentina walipata msukosuko kwenye Nusu Fainali yao na Netherlands kwa kwenda Dakika 120 wakiwa Sare 0-0 na hatimae kufuzu kwa Mikwaju ya Penati 4-2 hapo Jumatano.
Fainali hii ya Jumapili inakumbushia Fainali za Miaka ya 1986 na 1990 miamba hii ilipopambana.
Fainali hizo ndizo mara ya mwisho kwa Nchi hizo kutwaa Kombe la Dunia wakati Argentina ilipoifunga West Germany huko Mexico Mwaka 1986 na Germany kuifunga Argentina Mwaka 1990 na kuwa Mabingwa wa Dunia.
Tangu wakati huo, Argentina na Germany hazijatwaa tena Kombe la Dunia.
Kwenye Mechi za hivi karibuni kwenye Kombe la Dunia kati ya Argentina na Germany, Kikosi cha Joachim Loew ndio kimekuwa kidedea kwa kuishinda Argentina kwa Penati Mwaka 2006 kwenye Mashindano yaliyochezwa Nchini Germany na huko Afrika Kusini Mwaka 2010, Germany iliibamiza Argentina 4-0.
Ikiwa Germany itaishinda Argentina hiyo Jumapili, hii itakuwa mara ya kwanza kwa Nchi ya Ulaya kutwaa Ubingwa Bara la Marekani ya Kusini.
BRAZIL-SAFARI YA FAINALI:
ARGENTINA
HATUA
GERMANY
v Bosnia 2-1
KUNDI
v Portugal 4-0
v Iran 1-0
KUNDI
v Ghana 2-2
v Nigeria 3-2
KUNDI
v USA 1-0
v Switzerland 1-0
RAUNDI YA PILI
v Algeria 2-1
v Belgium 1-0
ROBO FAINALI
v France 1-0
v Netherlands 0-0 [Penati 4-2]
NUSU FAINALI
v Brazil 7-1

TATHMINI:
Bila shaka, baada ya kuibamiza Brazil Bao 7-1, Germany wataingia kwenye Fainali hii wakiwa kifua mbele kwa kujiamini.
Staili ya Germany ni lile Soka ambalo limetulia lenye pasi rahisi si zile nyingi kama Tiki-Taka ya Spain lakini upenyo ukipatikana tu ni wepesi wa kufanya shambulizi la nguvu na kustukiza.
Kocha wa Germany, Joachim Loew, alibadilisha mbinu na mfumo huko Brazil kwa kuamua kumrudisha Nahodha wake Philipp Lahm kwenye nafasi yake ya asili ya Fulbeki wa Kulia kutoka Kiungo Mkabaji na kwenye Kiungo kuweka Mtu 3, Toni Kroos, Bastian Schweinsteiger na Sami Khedira
Kwa upande wa Argentina, ukimwondoa Lionel Messi, mara nyingi Wachezaji wao wengine hawaonyeshi kuwa tishio.
Tangu mwanzoni mwa Mashindano haya, Messi amekuwa akiibeba Timu kwa ama kufunga Bao zao muhimu au kuchangia katika kufunga Bao zao za ushindi.
Ukimwondoa Angel di Maria, ambae kidogo alionyesha uhai lakini akaumia na pengine hatacheza Fainali hii, wanao Ezequiel Lavezzi na Gonzalo Higuain ambao ufungaji wao umekuwa adimu au hamna kabisa.
Licha ya ile imani ya Wachambuzi wengi kwamba Difensi ya Argentina ni ‘nyanya’, Nchi hiyo imeonyesha umahiri mkubwa kwa kuweza kucheza Mechi 4 bila kufungwa hata Bao.
Difensi yao ya Mtu 4, Zabaleta, Demichelis, Garay na Rojo, imekuwa ikilindwa vilivyo na Kiungo Mkabaji Javier Mascherano ambae ameibuka kuwa mmoja wa Nyota waliong’ara mno huko Brazil kwa mchango wake mkubwa.
Kocha wa Argentina, Alejandro Sabella, atakuwa akisali kuomba Difensi yake iweze kuhimili vishindo vya ‘Mashine ya Kijerumani’ huku akiomba sana Messi ang’are japo kwa sekunde moja tu ili awape Bao la ushindi.
DONDOO MUHIMU:
Uso kwa Uso
Argentina-Ushindi 9
Germany-Ushindi 6
Wafungaji wao Bora huko Brazil
Germany: Thomas Muller (5)
Argentina: Lionel Messi (4)
Takwimu
-Huko Brazil, Argentina imefunga Bao 8 wakati Germany ina Bao 17.
-Germany sasa wameipiku Brazil na kuwa ndio Wafungaji Bora Fainali za Kombe la Dunia wakiwa na Mabao 223.

REFA: Nicola Rizzoli [Italy]
+++++++++++++++++++++++++++++++
Kumbukumbu
Argentina 3 West Germany 2, Fainali Kombe la Dunia, Mexico 1986
Fainali za Mwaka huo zitakumbukwa kwa ajili ya Maradona wakati Germany ilipotanguliwa Bao 2-0 mapema Kipindi cha Pili.
Germany, wakiongozwa na Franz Beckenbauer, wakajitutumua na kufanya Gemu iwe 2-2 kwa Bao za Karl-Heinz Rummennigge na Rudi Voller huku Dakika zikibaki 10.
Huku kila Mtu akitegemea Mechi inaenda Dakika za Nyongeza 30, Maradona akatoa pande safi kwa Jorge Burruchaga aliekutana uso kwa uso na Kipa Schumacher na kupiga shuti lililompita Kipa huyo na kuipa Argentina ushindi wa Bao 3-2.
Hicho kilikuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Germany kwenye Fainali ya Kombe la Dunia na ndio mara ya mwisho kwa Argentina kuwa Bingwa wa Dunia.
Argentina 0 West Germany 1, Fainali Kombe la Dunia, Italy 1990
Argentina na Germany zilikutana tena Fainali iliyoufuata huko Stadio Olympico Jijini Rome na Germany kulipa kisasi.
Mechi hiyo ilishuhudia Mchezaji wa Argentina Pedro Monzón akitolewa kwa Kadi Nyekundu na kuweka Rekodi ya kuwa Mtu wa kwanza kutolewa nje kwenye Fainali.
Bao la ushindi la Germany lilipatikana kwa Penati iliyotolewa kwa faulo dhidi ya Rudi Voller na Andreas Brehme kufunga Penati hiyo.
KOMBE LA DUNIA
RATIBA
**Saa za Bongo
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014
SAAMECHIKUNDIUWANJA 2200Germany v ArgentinaFAINALIEstadio do Maracanã, Rio de Janeiro
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014
SAAMECHIKUNDIUWANJA
2200Germany v ArgentinaFAINALIEstadio do Maracanã, Rio de Janeiro
WENYEJI Brazil wamemaliza Fainali za Kombe la Dunia kwa huzuni na fedheha kubwa baada ya kuikosa hata Nafasi ya Tatu walipotandikwa Bao 3-0 na Netherlands huko Mjini Brasilia na kuwafanya Mashabiki wao wawazomee mwishoni mwa Mechi. Lakini Brazil waliingia Uwanjani kwa kushangiliwa na hasa Neymar, ambae ni Majeruhi, kuingia huku akiwa amevaa Jezi na kupokewa kwa shangwe kubwa.

Wakichezesha Kikosi kilichobadilisha Wachezaji 6 toka kile kilichobamizwa 7-1 kwenye Nusu Fainali na Germany, Brazil, kwa mara nyingine tena walionyesha udhaifu mkubwa wa Difensi yao ambao ulitoa zawadi ya ushindi kwa Netherlands.
Netherlands, ambao kwenye Mechi zao za Robo Fainali na Nusu Fainali walishindwa kufunga hata Bao moja baada zote kwisha 0-0 na kuamuliwa kwa Mikwaju ya Penati, walipata Bao lao la Kwanza Dakika ya Tatu tu kupitia Penati ya Robin van Persie.
Penati hiyo ilitoka kwa Nahodha wao Thiago Silva, ambae ndio kwanza ametoka Kifungo cha Mechi moja, alipomvuta Arjen Robben na kunusurika kupewa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 16, David Luiz nae akatoa ‘boko’ jingine kwa kupiga Kichwa kibovu cha kuokoa na Mpira kutua kwa Daley Blind aliefunga Bao la Pili.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO:
-Hii ni mara ya kwanza tangu 1940 kwa Brazil kufungwa Mechi 2 mfululizo Nyumbani kwao. Mwaka 1940, walifungwa 3-0 na Argentina na kisha 4-3 na Uruguay.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Bao la Tatu la Netherlands lilifungwa katika Dakika za Majeruhi na Wijnaldum na kuwapa Netherlands ushindi wa 3-0 na kukamata Nafasi ya Tatu.
Leo Usiku, Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2014 zinakamilika kwa Mechi ya Fainali kati ya Argentina na Germany.
VIKOSI:
Brazil:
12 Julio César
23 Maicon
14 Maxwell
17 Luiz Gustavo (Fernandinho - 45')
03 Thiago Silva
04 David Luiz
16 Ramires (Hulk - 73')
08 Paulinho (Hernanes - 57')
21 Jo
19 Willian
11 Oscar
Netherlands:
01 Cillessen (Vorm - 93')
15 Kuyt
05 Blind (Janmaat - 70')
04 Martins Indi
02 Vlaar
03 de Vrij
16 Clasie (Veltman - 90')
08 de Guzmán
20 Wijnaldum
09 van Persie
11 Robben
REFA: Djamel Haimoudi [Algeria]


MANCHESTER UNITED imetangaza Mechi maalum Uwanjani Old Trafford hapo Jumanne Agosti 12 ambapo watacheza na Valencia ya Spain na pambano hilo kuitwa ‘REUNITED 14’.
Hiyo itakuwa Mechi ya Kwanza kabisa kwa Meneja mpya wa Man United, Louis van Gaal akisaidiwa na Meneja Msaidizi Ryan Giggs, Uwanjani hapo.
Pamoja na hao, pia Mechi hiyo inaweza kuwa ya kwanza kabisa Uwanjani Old Trafford kwa Wachezaji wapya Ander Herrera na Luke Shaw.
Pamoja na Mechi hiyo, Mashabiki wote na Familia zao ambao watahudhuria watapata burdani mbalimbali ili kuwahamsisha kwa ajili ya Msimu mpya wa 2014/15.
Mechi hiyo itakuja mara baada ya Ziara ya Kabla Msimu mpya huko Marekani ambapo Man United watacheza Mechi 4.
Hivi sasa Kikosi cha Man United, bila ya Wachezaji walioshiriki Kombe la Dunia huko Brazil na Nchi zao, kimeanza Mazoezi chini ya Ryan Giggs huko Jijini Manchester kwenye Kituo chao cha Mazoezi cha AON Training Complex.
Man United wataruka hapo Julai 18 kuelekea huko Marekani na kupiga Kambi huko California kabla ya kucheza Mechi yao ya Kwanza huko USA hapo Julai 23 dhidi ya LA Galaxy kugombea Chevrolet Cup ndani ya Rose Bowl, Pasadena.
USA-ZIARA YA KABLA MSIMU MPYA:
[Zote Nchini Marekani]
Manchester United v LA Galaxy
Chevrolet FC Cup
Jumatano 23 Julai 2014, Rose Bowl, Pasadena
Manchester United v AS Roma
International Champions Cup
Jumamosi 26 Julai 2014, Sports Authority Field, Denver
Manchester United v Inter Milan
International Champions Cup
Jumanne 29 Julai 2014, FedEx Field, Washington DC
Manchester United v Real Madrid
International Champions Cup
Jumamosi 2 Agosti 2014, Michigan Stadium, Ann Arbor

HII ni Mechi ambayo kila upande, baada kuhuzunishwa na kushindwa kutinga Fainali, hautaki kucheza lakini hulazimika kucheza ili mradi kukamilisha Ratiba tu.
Kocha wa Netherlands, Louis van Gaal, ambae Timu yake ilibwagwa kwenye Nusu Fainali na Argentina kwa Mikwaju ya Penati 4-2, ameshasema kuwa si haki kwa Timu kucheza Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu wa Kombe la Dunia wakati kila mmoja alikuja kubeba Kombe la Dunia.

Lakini kwa Wenyeji Brazil inaelekeo lengo lao ni tofauti kabisa hasa baada ya kufedheheshwa Nyumbani kwao kwa kushindwa kuingia Fainali na kutwaa Kombe la Dunia lakini pia hilo limetokea baada ya kuaibishwa mno walipotwangwa Bao 7-1 na Germany kwenye Nusu Fainali.

Baada ya maafa hayo, kila Mtu kwenye Kambi ya Brazil ametaka wajifariji japo kidogo kwa kuifunga Netherlands na angalau kushika nafasi ya Tatu.

Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari, ameshasema wao watacheza kulinda hadhi ya Jezi ya Timu ya Taifa.


Staa wao mkubwa, Neymar, ambae alivunjwa Mfupa wa mdogo wa Mgongoni kwenye Mechi ya Robo Fainali na Colombia na hivyo kushindwa kucheza Mechi na Germany na kuondolewa Kambini, amerudi Kambini mwa Brazil ili kuwahamasisha wenzake kwa ajili ya Mechi na Netherlands.

Neymar amesema: “Tulipata nafasi ya kuwa Mabingwa Nchini kwetu na tukashindwa. Hatukuonyesha jinsi Soka la Brazil lilivyokuwa zuri, la juu na kuvutia lakini lazima tuitazame Mechi hii ya mwisho kama Fainali. Ushindi hautafuta uchungu tunaosikia hii Leo lakini ni muhimu.”

Ingawa Neymar hataweza kucheza lakini Brazil watamkaribisha tena Nahodha wao Thiago Silva ambae hakucheza Mechi na Germany alipokuwa akitumikia Kifungo cha Mechi moja baada kuzoa Kadi za Njano mbili.

Uso kwa Uso:

Mechi: 11

Brazil: Ushindi 3

Netherlands: Ushindi 3

Sare: 5

VIKOSI VINATARAJIWA:

Brazil: Cesar, Marcelo, Silva, Alves, Luiz, Gustavo, Fernandinho, Hulk, Oscar, Fred, Willian

Netherlands: Cillessen; Indi, Vlaar, Vrij; Blind, Wijnaldum, Guzman, Kuyt; Sneijder; Robben, Van Persie.
REFA: Djamel Haimoudi [Algeria]
KOMBE LA DUNIA
RATIBA
**Saa za Bongo
MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Brazil v Netherlands
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2200
Germany v Argentina
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro