Christino Ronaldo aliifungia Ureno goli la dakika za mwisho na kuipa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Denmark, katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Euro 2016 kundi I.Ureno ambayo ilikuwa na machungu ya Kupoteza mchezo wake dhidi ya Albania kwa kipigo cha bao 1-0 nyumbani,iliuanza mchezo kwa nguvu na kufanya mashambulizi, ingawa wenyeji nao walipata nafasi nzuri kipindi cha kwanza hasa kwa shambulizi la Michael Krohn-Dehli ambalo liligonga mwamba.
Ronaldo aliipatia timu yake bao la ushindi dakika ya 95 kufuatia shuti kutoka kwa Ricardo Quaresma na kuzima ndoto za Denmark waliokuwa wenyeji kupata sare.
kwa matokeo hayo Ureno imechupa toka nafasi ya mwisho mpaka a tatu ikiwa na pointi 3 nyumaya Denmark baada ya kucheza mechi 2, kushinda 1 na kupoteza 1.
0 comments:
Post a Comment