mpya
nyumbani
VPL: AZAM YAIBURUZA MBEYA CITY NYUMBANI, MTIBWA YASHIKWA.
Michezo mingi ya ligi kuu Tanzania bara imechezwa leo katika
viwanja tofauti tofauti,Azam walikuwa mjini Mbeya kuvaana na Mbeya City
katika mchezo uliokuwa mkali na wenye ushindani wa hali ya juu sana ila
wameweza kuibuka na ushindi mdogo wa bao 1-0 ambalo limepachikwa kimiani
na nahodha wao Aggrey Moris.
Matokeo ya michezo mingine ni Morogoro derby kati ya Mtibwa Sugar na
Polisi ya Morogoro ambazo zimetoka nguvu sare bila ya kufungana.
Na huko mkoani Mtwara katika uwanja wa Nangwanda timu ya Ndanda FC
imekubali kichapo cha mabao 3-1 toka kwa JKT Ruvu. Mabao ya JKT Ruvu
yalifungwa na Juma Ndeule, Abrahman Mussa na Thomas Matayo.
0 comments:
Post a Comment