Kaseja alipokuwa akisaini mkataba kuingia Yanga Mwaka jana |
Kipa wa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam amewasilisha barua ya taarifa ya kuvunja mkataba ambao umebakiza mwaka mmoja kumalizika. Katika barua hiyo Kaseja amedaiwa kutoa sababu za uvunja mkataba huo kuwa ni kuvunjwa kwa makubaliano ya mkataba huo kiubwa kikiwa ni ushindwa kulipwa kwa sehemu ya malipo wa mkataba huo yenye thamani ya milioni 20.
Katika mkataba aliousaini Kaseja Novemba mwaka jana, Kaseja alipaswa kulipwa kiasi cha Milioni 20, na kiasi kilichobaki kilipaswa kulipwa januari 15 mwaka huu, kitu ambacho hakijatimizwa mpaka sasa.
Kaseja amesema amevunja mkataba na Yanga na anatafuta klabu nyingine.Kauli hiyo ya Kaseja imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba Bw.Hans Poppe kusema kuwa milango ipo wazi kwa mchezaji huyo anakaribishwa kurudi msimbazi kama akiataka kwani Msimbazi ni Nyumbani kwao, hali inayotoa ishara kuwa huenda Kaseja akarudi Msimbazi kumalizia soka lake.