Thomas Mueller akifunga goli la kwanza. |
Hatimaye ile ndoto ya kombe kutopanda ndege imezima hapo jana huko Brazil, baada ya wenyeji hao kupata kipigo cha haja cha jumla ya magoli 7-1 kutoka kwa wajerumani. Magoli ya Ujerumani ambao mpaka dak. 30 za kipindi cha kwanza walishafunga magoli 5 yalifungwa na Mueller dak.11,Klose dk.23,Kroos dk.24,26,Khedira 29,Schuerrle dk. 69,79. Huku lile la Brazil la kufutiamachozi likifungwa na Oscar dak. ya 90.
REKODI ZAVUNJWA:
Katika hatua nyingine mchezaji nguli wa Ujerumani Miroslav Klose's ameweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika michuano hiyo kwa kufikisha jumla ya magoli 16,akimpiku Ronald de Lima wa Brazil mwenye magoli 15.

Pia Ujerumani imeweka rkodi mpya ya kufunga magoli mengi zaidi katika hatua ya nusu fainali, pamoja na rekodi ya kuongoza kwa magoli mengi katika kipindi cha kwanza, ambapo hapo jana waiongoza kwa magoli 5-0 mpaka mapumziko.
Toni Kroos akiifungia Ujerumani goli la tatu.
Ubao wa matangazo ulivyosoma jana, ingekuwa Sokoine Mbeya vibao vingekuwa vimeisha. |
Maumivu na machozi. |
Klose ameandika rekdi mpya hapo jana kwa kuwa mfungaji bora wa wakati wote katika kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment