Wengi wanadai Wenyeji Brazil wamesuasua
hadi kufikia Nusu Fainali ya Kombe la Dunia ambapo Jumanne Usiku
watawavaa Germany huko Estadio Mineirão, Belo Horizonte lakini pia hata
hiyo Germany, huko Brazil, nayo inasemwa imefanya vyema kwa vipindi tu.
PATA TATHMINI/DONDOO/VIKOSI VYA MTANANGE HUU:
BRAZIL v GERMANY
-Jumanne Julai 8, Saa 5 Usiku, Bongo Taimu
Hii itakuwa ni mara ya pili tu kwa
Brazil na Germany kukutana kwenye Kombe la Dunia wakati watakapocheza
Nusu Fainali huko Estadio Mineirão Mjini Belo Horizonte Nchini Brazil.
Mara pekee waliyokutana ni Mwaka 2002
kwenye Fainali ya Kombe la Dunia huko Yokohama, Japan na Brazil kushinda
Bao 2-0, kwa Bao za Ronaldo, na kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya 5,
hiyo ikiwa mara yao ya mwisho na wakati huo Kocha wao ni huyu huyu wa
sasa Luiz Felipe Scolari.
Brazil
Kwenye Fainali hizi, Brazil walianza
pole pole lakini katika Robo Fainali, walipocheza na Colombia, kwa muda
mwingi walionyesha ufundi, bidii, nguvu na ari ya kusaka ushindi kwa
kila hali.
Lakini Mechi hiyo ilizaa pigo kubwa kwao
baada kuumia kwa Nyota wao Neymar, na, bila shaka, Kocha Luiz Felipe
Scolari, kwa kumkosa Neymar na pia Nahodha wao Thiago Silva kutokana na
kufungiwa Mechi moja, ameshapata mbinu za kuziba mapengo yao.
Ingawa Wachambuzi wengi wanadai Brazil
hii si maridhawa lakini kila hatua waliyopiga kufikia Nusu Fainali ni
kuwajengea hisia zaidi na kuwapa imani kubwa kwamba hii ni hatima yao
kutwaa Kombe la Dunia Nyumbani kwao wenyewe baada ya kukosa kufanya
hivyo kwenye Fainali za Mwaka 1950 walipofungwa 2-1 na Uruguay Uwanjani
kwao wenyewe Maracana, Rio de Janeiro.
Brazil walianza kampeni yao kwa kuifunga
Croatia, kutoka Sare na Mexico, kuitwanga Cameroon 4-1 lakini
walihitaji Mikwaju ya Penati kuibwaga Chile kwenye Raundi ya Pili.
Katika Robo Fainali, dhidi ya Colombia,
Brazil ndio walionyesha dalili za kuwa ni Timu imara huku Washabiki wao
wakidhihirisha wataleta mchango mkubwa wa kuwahamasisha mno kwenye Mechi
yao ya Nusu Fainali.
++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-Brazil wametinga Fainali mara zao zote 6 walizofika Nusu Fainali.
-Germany ni Nchi ya kwanza kufika Nusu Fainali mara 4 mfululizo.
++++++++++++++++++++++
Ujerumani
Kama kawaida yao, ni ile ile
mashine halisi ya Kijerumani ambayo Siku zote huleta matokeo kwa uhodari
wao wa kupigania kila Mpira tangu mwanzo hadi mwisho.
Hata hivyo, Kocha Joachim Low anayo kazi
ya kuhakikisha Difensi yao inaacha kutoa mianya hasa kwa mtindo wao
hatari wa kupanda juu karibu ya mstari wa kati ambapo wakipitwa Kipa wao
Manuel Neuer hulazimika kucheza staili ya ‘Kipa Beki Mfagiaji!’
Kikosi cha Low kinaundwa na Wachezaji wengi kutoka Bayern Munich na hilo limeleta uimara mkubwa kwa Timu kucheza kitimu zaidi.
Kwenye Benchi lao wanae Straika mkongwe
Miroslav Klose ambae aliingizwa kuiokoa Germany walipokuwa nyuma kwa Bao
2-1 walipocheza na Ghana hatua ya Makundi na kufunga Bao la kusawazisha
lililomfanya aifikie Rekodi ya Ronaldo wa Brazil ya kufunga Jumla ya
Bao 15 kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Uso kwa Uso
-Mechi 21: Brazil wameshinda Mechi 12, Germany 4, Sare 5
Mechi za hivi karibuni:
-10 Agosti 2011: Germany 3-2 Brazil- Kirafiki, Mercedes-Benz Arena
-25 Juni 2005: Germany 2-3 Brazil- Fifa Kombe la Mabara Nusu Fainali, Frankenstadion, Nuremberg
-7 Sep 2004: Germany 1-1 Brazil- Kirafiki, Berlin
-30 Juni 2002: Brazil 2-0 Germany- 2002 Fainali Kombe la Dunia, International Stadium, Yokohama
-24 Julai 1999: Brazil 4-0 Germany- Kombe la Mabara Makundi, Estadio Jalisco, Guadalajara
VIKOSI VINATARAJIWA:
KOMBE LA DUNIA
RATIBA
**Saa za Bongo
NUSU FAINALI JUMANNE, JULAI 8, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Germany v Brazil [61] |
NUSU FAINALI |
Estadio Mineirão, Belo Horizonte |
0 comments:
Post a Comment