LIGI KUU BARA: YANGA YAPETA, PRISONS, MBEYA CITY HALI MBAYA, MTIBWA NA KAGERA YAHAIRISHWA.



BEKI WA MGAMBO AKIJARIBU KUMDHIBTI MSHAMBULIAJI WA YANGA, JAJA RAIA WA BRAZIL WAKATI TIMU HIZO ZILIPOKUTANA LEO KWENYE MCHEZO WA LIGI KUU BARA KWENYE UWANJA WA TAIFA NA WENYEJI KUSHINDA KWA MABAO 2-0. CHEKI PICHA ZAIDI.









Mabao mawili ya Simon Msuva leo yamewapa wanajangwani ushindi wa nyumbani dhidi ya Mgambo JKT katika uwanja wa taifa. Msuva ambaye leo amerejea baada ya kuwa majeruhi alikuwa mwiba wa safu ya ulinzi ya Mgambo na kufanikiwa kufunga goli la kwanza dakika ya 73 akitokea benchi baada ya akimbadili Niyonzima. Msuva alifunga goli hilo akitumia mwanya wa uzembe wa kipa aliyeshindwa kutokea akizani Msuva ameotea.
Daika ya 88 Msuva aliipatia timu yake goli la pili aiunganisha pasi ya Dilunga, na kuihakikishia timu yake pointi 3 muhimu baada ya kupata kipigo wiki iliyopita kutoka kwa Kagera.


MTIBWA VS KAGERA SUGAR: Katika Mechi nyingine iliyoikutanisha miamba ya soka Kagera Sugar na Mtibwa Sugar imevunjika na kuhairishwa mpaka kesho baada ya mvua kubwa kunyesha katika Uwanja wa Manungu Turiani, Morogoro, wakati mechi ikivunjika Mtibwa walikuwa wakiongoza kwa goli moja lililofungwa na Ame Ally.



MBEYA CITY, PRISONS  HALI MBAYA: Mbeya city imeendeleza rekodi ya matokeo mabaya baada ya leo hii kufungwa goli 1-0 na Stand United katika Uwanja wa Kambarage Mkoani Kagera, huku ndugu zao Prisons nao wakiambulia kichapo kama hicho cha bao 1-0 kutoka kwa Polisi Morogoro, goli la washindi liifungwa na Mkongwe Danny Mrwanda.
CREDITS: PICHA SOURCE: SALEHE JEMBE BLOG.

0 comments:

Post a Comment