Okwi akishangilia goli lake leo. |
Okwi aifanya Yake. |
Kocha Patrick Phiri akimpongeza Okwi. |
Mashabiki wa Simba wakishangilia mara baada ya 'Kuvunja mwiko' wa kutokushinda |
Najua mashabiki wengi wa Simba walikua wanasikilizia sana hii mechi
ya leo kama ilivyoahidiwa na club hiyo na kweli kitu kikajibu ambapo
mpaka Full Time ilikua Simba 1 – 0 Ruvu Shooting.
Bao pekee lililoipa Simba ushindi lilifungwa na mchezaji wa kimataifa toka Uganda Emmanuel Okwi ambaye alifunga bao hilo kwenye dakika ya 78 ya mchezo huo zikiwa zimesalia dakika 12 tu kabla ya mchezo kumalizika.
Simba
walitawala mchezo huo tangu mwanzo hadi mwisho wakitengeneza nafasi
nyingi za kufunga ambazo hata hivyo walishidnwa kuzitumia huku
washambuliaji wake wakikosa umakini walipokuwa wakifika langoni.
Ruvu Shooting nao walijitahidi kuleta presha langoni mwa Simba lakini
walishindwa kabisa kufanya kile ambacho timu tano zilizocheza na Simba
kabla ya mchezo huu wa leo zimeweza kukifanya, yani kuifunga.
Ushindi huu unawafanya Simba kufikisha pointi tisa baada ya kushinda
mchezo mmoja huku wakitoka sare sita na wanapanda toka nafasi ya kumi
mpaka nafasi ya sita.
Matokeo haya pia yanamaanisha kuwa Simba wanaendelea kuwa moja kati
ya timu mbili ambazo hadi sasa hazijaweza kupoteza mchezo wowote huku
timu nyingine ikiwa Mtibwa Sugar.
0 comments:
Post a Comment