Juventus 7-0 Parma: Brilliant Bianconeri run riot in Turin 
Fernando Llorente, Carlos Tevez na Alvaro Morata wamefunga magoli mawili kila mmoja huku Stephan Lichtsteiner akifunga moja kuisaidia Juventus kuiangamiza Parma kwa mabao 7-0 .
Mabingwa hao wa Serie A ambao walitumia nguvu nyingi uwashinda Olimpiacos katika ligi ya mabingwa Ulaya siku ya  Jumanne iliyopita, hawakuwa na kazi ngumu leo, ambapo walionekana kuwazidi wapinzani wao kwa kiasi iubwa mno. 

Kwa matokeo hayo Juve wameendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 28, wakiwa wamecheza michezo 11, wameshinda michezo 9 wamepoteza 1, na kutoka sare 1.