LIGI KUU BARA: MTIBWA YABANWA NA KAGERA SUGAR


Mtibwa Sugar na Kagera Sugar, leo zimemalizia kiporo chao cha pili kwa kutoka sare ya bao 1-1.

Kama unakumbuka jana mchezo ulivunjika wakati Mtibwa Sugar ikiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Ame Ali.
Lakini mvua kubwa ikalazimu pambano liahirishwe na leo asubuhi kwenye uwanja wa Manungu, dakika 45 zilizobaki zikamaliziwa.
Kagera ikapata bao lake kusawazisha kupitia kwa Rashidi Mandawa katika dakika ya 57.
Sare hiyo ni ya tatu kwa Mtibwa Sugar ambayo imeshinda mara nne na kuendelea kubaki kileleni.
 
Credits: Saleh Jembe.

0 comments:

Post a Comment