LA LIGA: REAL MADRID YAUA 5-1, RONALDO KAMA DAWA; BARCA YASHINDA PIA.

Real Madrid 5-1 Rayo Vallecano: Bale sparks Blancos rout 

Timu ya Real Madrid ya Hispania jana usiku imetoa tena kipigo cha haja kwa timu ya Rayo Vallecano katika La Liga.Mechi hiyo ambayo ilichezwa uwanja wa Santiago Bernabeu, nyummbani kwa Madrid magoli ya washindi yalifungwa na Galeth Bale dak.9, Sergio Ramos dak.40, T.Kroos dak.55, K.Banzema dak. 59 na lile la mwisho likafungwa na mkali wa nyavu Christiano Ronaldo dak. 83.
Goli la kufutia machozi wa Rayo lilifungwa na Bueno dakika ya 44.

BARCELONA VS ALMERIA: Katika Mechi nyingine ya La liga wapinzani wakubwa wa Real Madrid Barcelona walipata ushindi wa ugenini wa magoli 2-1 dhidi ya Timu ya Almeria, ahsante kwa magoli ya Neymar dak. ya 73 na Alba dak. ya 82.
Barcelona waliokuwa nyuma ya goli moja lililofungwa na T.Bifouma dak.37 walipigana kipindi cha pili na kujitahidi kutawala mchezo.
Almeria 1-2 Barcelona: Neymar and Alba rescue visitors

Kwa Matokeo hayo Real Madrid wameendelea kushika usukani wa Ligi baada ya kucheza michezo 11 na kufiisha pointi 27, huku Barcelona wakishika nafasi ya pili kwa kucheza michezo 11 na kupata pointi 25.

0 comments:

Post a Comment