SIMBA KUANZA MAZOEZI DAR THEN ZANZIBAR.

 
Simba itaanza mazoezi jijini Dar es Salaam kwa zaidi ya siku tano kabla ya kuhamia visiwani Zanzibar.
Kikosi hicho cha Msimbazi kitaanza mazoezi bila ya kocha wake, Zdravko Logarusic ambaye anatarajiwa kuwasili Jumatano.
Loga yuko nyumbani kwao Croatia ambako amekwenda kwa ajili ya mapumziko na Simba itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Selemani Matola.
Loga ataungana na timu siku chache kabla ya safari ya Zanzibar ambako Simba itaweka kambi huku ikiangalia uwezekano wa kuiboresha kambi hiyo.

0 comments:

Post a Comment