Hii ni Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Dunia, kufuatia ile ya Wenyeji Brazil na Germany inayochezwa Jumanne Usiku.
PATA TATHMINI/DONDOO/VIKOSI VYA MTANANGE HUU:
Nchi
hizi zina Historia ndefu kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambayo
inaanzia Mwaka 1974 kwa Netherlands kuitwanga Argentina 4-0 huko
Gelsenkirche, Ujerumani lakini Miaka Minne baadae Argentina, wakiwa kwao
Buenos Aires Uwanja wa River Plate, waliitwanga Netherlands Bao 3-1
katika muda wa Nyongeza , baada Sare ya 1-1 katika Dakika 90, na kutwaa
Ubingwa wa Dunia.
Safari hii, huko Brazil, Argentina na
Netherlands zote zimeonyesha Soka la kuridhisha na wote kubakisha Mechi 2
tu ili kutwaa Ubingwa wa Dunia huku Argentina wakisaka Taji la 3 na
Netherlands lao la kwanza.
Argentina
Kama walivyokuwa Wenyeji Brazil na Staa wao Neymar, ni siri ya wazi matumaini na matarajio ya Argentina yapo kwa Lionel Messi.
Lakini, kwenye Raundi za Mtoano,
Wachezaji wengine waliibuka na kuchukua jukumu la Messi pale Angel Di
Maria alipofunga Bao la ushindi walipoibwaga Switzerland kwenye Raundi
ya Pili na Gonzalo Higuain alipofunga Bao la ushindi na kuitosa Belgium
kwenye Robo Fainali.
Lakini pia Argentina wanao Wachezaji
wengine wapinaji ngangari ambao ni pamoja na Pablo Zabaleta, Javier
Mascherano na Ezequiel Garay.
Hata hivyo, Wachambuzi wengi wanaunga
mkono kauli ya Kocha wa Belgium, Marc Wilmots, ambae baada ya kufungwa
na Argentina, alinena: “Hatukuvutiwa na Argentina. Kama Timu yangu
ingecheza kama wao, basi Wanahabari wa Nyumbani wangenikaanga! Argentina
ni Timu ya kawaida ila Mchezaji mmoja si kawaida!”
++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-Hii ni Nusu Fainali ya kwanza kwa Argentina tangu Mwaka 1990 ambapo walishinda na kutinga Fainali na kufungwa na West Germany.
-Kwenye Kombe la Dunia, Argentina na Netherlands zimekutana mara 4 na Netherlands kushinda mara 2, Argentina mara 1 na Sare 1.
Netherlands
Chini ya Kocha Louis van Gaal, Meneja
mpya wa Manchester United, Netherlands imekuwa tishio huko Brazil na
Kocha huyo kuonyesha umahiri mkubwa wa kubadilisha mbinu za papo kwa
hapo katikati ya Mechi zilizokuwa mrama kwao na kuleta ushindi.
Kwenye Mechi ya Raundi ya Pili, huku
wakiwa Bao 1-0 nyuma, Van Gaal alimtoa Nahodha wake na Mfungaji mkuu,
Robin van Persie, na kumwingiza Jans-Klaas Huntelaar ambae alitengeneza
Bao la kusawazisha la Wesley Sneijder la Dakika ya 88 na yeye mwenyewe
kufunga Bao la Pili kwa Penati ya Dakika ya 94 na kuichakaza Mexico 2-1.
Kwenye Robo Fainali, wakiwa Sare na
Costa Rica mwishoni mwa Dakika 120 za mchezo, Van Gaal aliamua kumtoa
Kipa wake Nambari Wani Cillessen na kumwingiza Kipa wa Akiba Tim Krul
kwa ajili ya Mikwaju ya Penati na kweli Krul alidaka Penati mbili na
kuifikisha Netherlands Nusu Fainali.
Netherlands walianza kwa kishindo huko
Brazil kwa kuwatandika waliokuwa Mabingwa wa Dunia, Spain, Bao 5-1
kwenye Mechi ya Kundi lao.
Wakiwa na Mafowadi Arjen Robben na Robin
van Persie, wanaolishwa na Wesley Sneijder, ambae pia ni Mfungaji
mzuri, Netherlands wanatarajiwa kuisumbua sana ngome dhaifu ya
Argentina.
Uso kwa Uso
-Mechi 8: Argentina wameshinda Mechi 1, Netherlands 4, Sare 3
Mechi za hivi karibuni:
-21 Juni 2006: Netherlands 0-0 Argentina- Kombe la Dunia 2006 FIFA Kundi C, Commerzbank Arena, Frankfurt
-12 Feb 2003: Netherlands 1-0 Argentina- Kirafiki, Arena Amsterdam
-31 Machi 1999: Netherlands 1-1 Argentina- Kirafiki, Arena Amsterdam
-4 Julai 1998: Argentina 1-2 Netherlands- Kirafiki, Olympic Amsterdam
VIKOSI VINATARAJIWA:
Argentina: Romero; Zabaleta, F Fernández, Garay, Basanta; Gago, Mascherano, Perez; Messi; Lavezzi, Higuaín
Netherlands: Cillessen; Blind, Indi , de Vrij, Vlaar, Janamat, Wijnaldum, Sneijder, Guzman, Robben, Van Persie
REFA: Cüneyt Çakir [Turkey]
KOMBE LA DUNIA
JUMATANO, JULAI 9, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Argentina v Netherlands [62] |
NUSU FAINALI |
Arena Corinthians, Sao Paulo |
MSHINDI WA TATU |
0 comments:
Post a Comment