Kiingilio
cha chini cha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas)
itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kitakuwa sh. 7,000.
Tiketi zinapatikana kwa mfumo wa
elektroniki kupitia M-PESA. Kiingilio hicho kwa ajili ya viti vya rangi
ya rangi ya chungwa, kijani na bluu. Viingilio katika maeneo mengine
vitatangazwa baadaye.
Mshabiki ili apate tiketi anatakiwa
kutumia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza 4, ingiza namba ya
kampuni 173399 kisha weka 7000 kwenye namba ya kumbukumbu ya malipo, na
weka
7000 kama kiasi cha bei ya tiketi na mwisho weka namba yao ya siri.
Baada ya hapo utapokea ujumbe wenye
orodha ya vituo vya MaxMalipo kwa ajili ya kuchukulia tiketi ukiwa na
namba ya uhakiki wa malipo yako.
Vituo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa
wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi
Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha daladala
Makumbusho), Sheer Illutions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka
makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).
Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop
Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege),
Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo,
Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge
(Posta), Uwanja wa Taifa) na ofisi za TFF (PPF Tower).
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment