ARGENTINA
imetinga fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Uholanzi kwa
penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 Uwanja
wa Sao Paulo nchini Brazil.
Sifa zimuendee kipa Sergio Romero aliyeokoa penalti mbili za Ron Vlaar na Wesley Sneijder na kuipeleka Argentina Fainali.
Arjen Robben na Dirk Kuyt pekee ndiyo walifunga penalti upande wa
Uholanzi, wakati za Argentina zilikwamisha kimiani na Maxi Rodriguez,
Sergio Aguero, Ezequiel Garay na Lionel Messi.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Cuneyt Cakir wa Uturuki, timu
zote zilishambuliana kwa zamu na sifa ziwaendee walinzi na makipa wa
timu hizo waliofanya kazi ya ziada kulinda nyavu.Shujaa wa matuta: Sergio Romero akiokoa penalti ya Ron Vlaar |
Arjen Robben alikuwa mwiba mbele ya safu ya ulinzi ya Argentina-
kadhalika na Lionel Messi alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Uholanzi
katika mchezo huo wa marudio ya fainali ya mwaka 1978.
Argentina sasa itamenyana na Ujerumani katika fainali ambayo jana iliwatoa wenyeji Brazil kwa mabao 7-1.
Kikosi cha Uholanzi kilikuwa: Cillessen, De Vrij, Vlaar, Martins
Indi/Janmaat dk46, Kuyt, De Jong/Clasie dk62, Sneijder, Wijnaldum,
Blind, Robben na Van Persie/Huntelaar dk96.
Argentina:
Romero, Zabaleta, Demichelis, Garay, Rojo, Biglia, Mascherano,
Lavezzi/Maxi Rodriguez dk101, Messi, Perez/Palacio dk81 na
Higuain/Aguero dk82.
Louis Van Gaal maahiri kwa mbinu akiwa ameyong'onyea. |
0 comments:
Post a Comment