Akizungumzia suala hilo Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Celestine Mwesiga amesema kwamba ni kweli FIFA wamemruhusu Okwi kuendelea kucheza soka wakati wenyewe wakishughulikia madai ya vilabu vya Simba SC na Etoile Du Sahel. "Kwanza ningependa kusema kwamba kazi ya FIFA kwenye hili suala ilikuwa sio kumruhusu mchezaji kuichezea au kutoichezea Yanga, hilo suala lipo chini ya shirikisho la soka nchini TFF. "Kilichotokea ni kwamba kulikuwa na malalamiko ya klabu ya Simba SC, juu ya uhalali wa uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi kutoka SC Villa kwenda Yanga na pili juu ya deni lao wanaloidai klabu ya Etoile Du Sahel. FIFA wameridhika na suala la uhamisho wa Okwi kwenda Yanga kwa maana ulifuata vigezo vyote na walipata ITC. "Pia kuhusu suala la deni la Simba wanayoidai Etoile,
FIFA imeeleza kwenye email yake kwamba suala lipo pale pale lakini halina uhusiano na suala la Okwi kusajiliwa Yanga. Sisi kama TFF tutaendelea kulifuatilia kiundani kuhakikisha Simba wanapata haki yao." Alipoulizwa kama suala la uhamisho wa Okwi kwenda Yanga halina tatizo lolote, hivyo Okwi ataruhusiwa kuichezea Yanga, Mwesiga alisema: "Kilichobaki sasa ni masuala ya ndani ya shirikisho. Tutaangalia kama mchezaji husika amekidhi vigezo vya kuweza kushiriki kwenye michuano mbalimbali hapa nchini, ikiwa atakuwa amekidhi basi tutakuwa hatuna kipingamizi chochote."
Hata hivyo mchezaji huyo attakiwa kusubiri kukamilika kwa taratibu zote zitakazomuweka huru na mikataba hiyo ya utata ,huku angalizo likitolewa kwa klabu ya Yanga na TFF kutofanya makosa kwani suala la mchezaji huyo bado lina utata, hasa kwa upande wa uhamisho wake.
Chanzo: Shafih Dauda.
0 comments:
Post a Comment