Gerald akifunga Penati ya ushindi kwa Liverpool jana. |
Timu za Manchester United na Arsenal jana zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bila kufungana.Licha ya kuanza mpira kwa kasi na kuonesha matumaini ya kuwepo magoli timu hizo ziliishia kwa droo tasa.
Vipindi vyote vilitawaliwa na timu zote mbili zikifanyiana mashamblizi ya zamu, huku nafasi chache zikikumbukwa ikiwepo ile ya Van Persie kukosa goli la wazi alipokuwa akitazamana na kipa wa Arsenal baada ya mabeki Per Mertesacker naWojciech Szczesny wa Arsenal kujichanganya.
Katika mechi nyingine Liverpool walitoka nyuma mara mbili na hatimaye kushinda dhidi ya Fulham, Fulham ndiyo waliotangulia kwa goli la kujifunga la Koure Toure ambaye jana hakuwa katika utulivu, Liverpool walisawazisha kwa goli la Sturridge,kisha Fulham wakaongeza kwa goli la Richardson, Liverpool walisawazissha tena dakika ya 80 kupitia kwa Coutinho aliyepiga shuti kali nje ya box.
Liverpool walijipatia goli la ushindi dakika za mwisho baada ya Sturridge kuangushwa eneo la hatari na peneati kupigwa na Steven Gerald ambaye hakufanya ajizi na kuipatia timu hiyo ushindi wa goli 3-2.
Totenham nao jana waliitambia New castle kwa goli 4-0 magoli ya Emanuel Adebayor dakika ya 19, na 82, Paulinho dk.53 na Nchadli dk.88. yalipa matumaini Totenham ya kuanza kuigia katika kinyang'anyro cha Top 4 kwa kufikisha pointi 50 nyuma ya Liverpool wenye pointi 53.
Kwa matokeo hayo arsenal wameendelea kuwepo nafasi ya pili wakiwa na pointi 56 nyuma ya vinara chelsea wenye pointi 57, nafasi ya tatu inashikwa na Man.City wenye pointi 54, ya nne ni Liverpool yenye Pointi 53, na Totenham wakikaribia kuingia Top 4 kwa pointi 50.
0 comments:
Post a Comment