Pamoja na kikosi chake cha Mwadui kushinda mabao 2-1 katika
mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Polisi Dodoma lakini Mwadui imeshindwa
kupanda Ligi Kuu Bara.
Ushindi huo uliifanya Mwadui inayonolewa na Julio kufikisha
pointi 31 ambazo zingeipandisha lakin Stand United iliyoshinda mabao 2-1 dhidi
ya Toto Afrika, ikafikisha pointi 29.
Lakini mwisho kabisa, Stand United ikabebwa na rufaa yake
dhidi ya Kanembwa ikafikisha pointi 32, na moja kwa moja ikapanda Ligi Kuu
Bara.
Kama si rufaa, Julio alikuwa amerejea Ligi Kuu Bara, hali
iliyofanya uongozi wa Mwadui kulalama kuhusiana na pointi hizo za rufaa.
0 comments:
Post a Comment