Fainali za Champions league zinaendelea leo ambapo kutakuwepo na mechi za leo ni Chelsea wakiwakaribisha Paris S Saint Germain, huku Borusia Dortmund wakiwa wenyeji wa Real Madrid. Katika mechi za kwanza Chelsea walipoteza kwa magoli 3-1 kutoka kwa PSG na leo watahitaji ushindi wa magoli mawili au zaidi ili kusonga mbele huku PSg wakihitaji droo ya aina yoyote au kufungwa goli moja. Chelsea inakabiliwa na Majeruhi kadhaa akiwepo Samuel Etoo ambaye mpaka sasa haijathibitika kama atakuwepo au hatokuwepo katika mechi, huku PSG wao wakikkabiliwa na majeruhi mmoja ambayo ni Zlatan Abrahamovic ambaye nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Edinson Cavani .
Upande wa mechi nyingine Real Madrid wanaifuata Borusia Dortmund nyumbani kwao katika uwanja wa
Signal-Iduna-Park,katika mechi ya kwanza BVB walilala kwa magoli 3-0 na
leo wanakibarua kigumu ili waweze kusonga mbele kwani watahitaji ushindi
wa magoli manne au zaidi ili waweze kusonga mbele.
0 comments:
Post a Comment