TP Mazembe ya Jamhuri ya Kodemokrasia ya Kongo (DRC) imeanza vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 na El Hilal Omduran usiku huu Uwanja wa Khartoum nchini Sudan.
Katika mchezo huo wa Kundi A, bao lililoizamisha Mazembe lilifungwa na Salah Al Jizoli dakika ya 51 akimalizia pasi ya Bakri Babeker.
Washambuliaji wote wawili wa Tanzania wa TPM walicheza, Mbwana Samatta akianza na Thomas Ulimwengu akitokea benchi dakika ya 66 kwenda kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.

Poleni vijana; Ulimwengu kulia na Samatta kushoto wote wamecheza leo Mazembe ikifungwa 1-0 Sudan
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kabisa wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu na mechi nyingine ya kundi hilo itachezwa keshokutwa kati ya AS Vita watakaoikaribisha Zamalek ya Misri mjini Kinshasa, DRC.
Mechi za Kundi B zitaanza kesho, Esperance ya Tunisia ikiikaribisha ES Setif ya Algeria na keshokutwa CX Sfaxien itaikaribisha Al Ahly Benghazi ya Libya nchini Tunisia.
Samatta na Ulimwengu wanatarajiwa kuondoka asubuhi kuja Dar es Salaam kujiunga na timu yao ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Zimbabwe, kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Morocco.

0 comments:
Post a Comment