TAIFA STARS ILIVYOLETA RAHA ZIMBABWE

Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakifurahia kuitoa Zimbabwe katika mechi ya mchujo kuwania tiketi nya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika jana Uwanja wa Taifa wa Harare, Zimbabwe baada ya sare ya 2-2 inayowafanya wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
Winga wa Taifa Stars, Simon Msuva akiwatoka wachezaji wa Zimbabwe
Kiungo wa Taifa Stars, Amri Kiemba akimtoka mchezaji wa Zimbabse
Kiungo wa Taifa Stars, Frank Domayo akiambaa na mpira
Thomas Ulimwengu akiwa ameanguka chini baada ya kuchezewa rafu na beki wa Zimbabwe
John Bocco akipambana na mchezaji wa Zimbabwe
Beki Oscar Joshua akimdhibiti mchezaji wa Zimbabwe, huku Frank Domayo kushoto akiwa tayari kutoa msaada
Beki wa Zimbabwe akiwa ameruka juu ya John Bocco kuondosha mpira kwenye himaya ya mshambuliaji huyo wa Taifa Stars
John Bocco akiwa amebebwa kwenye machela kutolewa nje baada ya kuumia. Hata hivyo, Bocco alirudi kuendelea na mchezo hadi akamaliza
Vikosi vya Zimbabwe na Tanzania vikiingia uwanjani
Mashabiki waliosafiri kutoka Dar es Salaam na wengine wakazi wa Harare waliojitokeza kuisapoti Taifa Stars jana

0 comments:

Post a Comment