Neymar ametua jijini
Barcelona, Hispania lakini hataanza kazi na kikosi cha Barcelona.
Badala yake atakwenda
kujichimbia Ibiza na kuendelea kula raha huku akiendelea na matibabu.
Daktari ameeleza, Neymar
amekuwa akipata nafuu haraka kuliko ilivyotegemewa kutokana na maumivu makali
baada ya kuvunjika sehemu ya uti wake wa mgongo.
Neymar aliumizwa na beki
wa Colombia, Juan Zuniga wakati wa michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika
hivi karibuni.
Akiongizana na mpenzi
wake, Bruna Marquezine, Neymar alitua Barcelona na mara moja ameondoka kwenda
Ibiza.
0 comments:
Post a Comment