Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwakabidhi vifaa Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Yanga George Simba |
Ikiwa ni
sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya
michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya msimu
wa 2014/15 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kavishe
aliongeza kuwa Vifaa ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi,
shin guards, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vitu vingine vingi
ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa
vyenye ubora wa hali ya juu.
Kilimanjaro
Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza
katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu
hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania.
Tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu,
tutahakikisha tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.
Kavishe
alisema kuwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga umelenga
kukuza soka la Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira
wakati na vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya
kimataifa.
Tunawashukuru
viongozi wa Simba na Yanga, mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau wote wa
mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo
ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu.
0 comments:
Post a Comment