LIVERPOOL YAANZA POA EPL

LIVERPOOL imeanza vizuri Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga mabao 2-1 Southamptons Uwanja wa Anfield jioni hii, ikicheza mechi ya kwanza ya ligi bila Luis Suarez iliyemuuza Barcelona.  Shukrani kwake, mshambuliaji wa kimataifa wa England, Daniel Sturridge aliyefunga bao la ushindi  dakika ya 79 na kumpa mwanzo mzuri Brenden Rodgers aliyeukosakosa kidogo ubingwa msimu uliopita akizidiwa kete na Manchester City.
La ushindi; Daniel Sturridge akiifungia Liverpool bao la ushindi leo 
Raheem Sterling alitangulia kuwafungia Wekundu hao dakika ya 23, kabla ya Nathaniel Clyne kuwasawazishia Watakatifu dakika ya 56.  Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Skrtel, Lovren, Johnson, Henderson, Gerrard, Lucas/Allen dk63, Sterling, Coutinho/Lambert dk76 na Sturridge. 
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Yoshida, Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Tadic/Long dk73, Ward-Prowse, S Davis/Isgrove dk82 na Pelle.

0 comments:

Post a Comment