KIKOSI CHA TAIFA
STARS KIMEWASILI SALAMA JIJINI MAPUTO KWA AJILI YA MECHI YAO YA
MARUDIANO DHIDI YA WENYEJI MSUMBIJI. MECHI YA KWANZA YA KUWANIA KUCHEZA
HATUA YA MAKUNDI KWENDA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA ILIMALIZIKA KWA SARE YA
MABAO 2-2 JIJINI DAR ES SALAAM. STARS IKIWA ANGANI
KUTOKA JOHANNESBURG, ILIJITOKEZA HITILAFU YA NDEGE, HALI ILIYOLAZIMISHA
NDEGE HIYO KUREJEA UWANJA WA KIMATAIFA WA OLIVER TAMBO NA KUFANYIWA
MATENGENEZO KWA DAKIKA 45 NA BAADAYE SAFARI IKAANZA TENA. KOCHA MART NOOIJ ANAAMINI KIKOSI KIKO KATIKA HALI NZURI KIKIJIANDAA NA MECHI HIYO INAYOTARAJIWA KUWA NGUMU. HATA
HIVYO STARS HAIJAFUNGWA KATIKA DAKIKA 90 IKIWA MAPUTO KATIKA MECHI
MBILI ZILIZOPITA, KAMA INAVYOONEKANA KWENYE PICHA IKIWASILI MAPUTO MWAKA
JUZI AMBAKO ILING'OLEWA KWA MATUTA BAADA YA SARE YA BILA KUFUNGANA DAR
NA MAPUTO. | | | | | | | | | | | | | | | | |
0 comments:
Post a Comment