Neymar alianza kuifungia Barca dakika ya 26, na Ivan Rakitic akafunga tena dak. ya 43, na kabla ya mapumziko Neymar akaifungia tena Barca bao la tatu katika dak ya 45.
Messi alifanikiwa kuandika historia yake ya kufunga goli la 400 katika dakika ya 62, na pia kufikisha goli la 248 katika ligi ya La Liga.
Alikuwa ni Neymar tena katika dak. ya 66 aliyeinyanyua Barca baada ya kumalizia kazi nzuri ya Messina kuandika bao la 5, dakika ya 82 Messi tena aliifungia Barca bao la 6 na kufikisha magoli 401 katika maisha yake ya soka.
Kwa ushindi huo Barca wameendelea kubaki kileleni wakiwa na point 16 na hawajapoteza mchezo hata mmoja katika msimu huu.
0 comments:
Post a Comment