LIGI YA MABINGWA: CHELSEA YABANWA NYUMBANI, BARCA YASHINDA KIBISHI,AS ROMA YAUA.

CHELSEA imelazimishwa sare ya nyumbani ya kufungana bao 1-1 na Schalke ya Ujerumani katika mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Kiungo Cesc Fabregas alitangulia kuifungia The Blues dakika ya 11 ingawa pia alionekana kuchezewa faulo kabla ya kufunga.


Katika mchezo mwingine bao pekee la Gerard Pique limeipa Barcelona ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Cypriots Apoel Nicosia ya Cyprus usiku huu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pique alifunga bao muhimu akimalizia mpira wa adhabu wa Lionel Messi katikati ya kipindi cha kwanza, lakini Apoel iliwabana vilivyo Barca licha ya kuongozwa na nyota wake Messi na Neymar mbele.
Mechi ya Sporting na Mribor:Luka Zahovic alitokea benchi kuinusuru Maribor kulala Sporting kwa kupata safe ya 1-1 kwa bao la dakika ya mwisho baada ya Luis Nani kutangulia kuwafungia wapinzani wao.


AS ROMA YAUA: MSHAMBULIAJI Gervinho na Nahodha mkongwe wa umri wa miaka 37, Francesco Totti wamefanya kazi nzuri usiku huu AS Roma ikiifumua CSKA Moscow mabao 5-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Olimpico. Gervinho amefunga mabao mawili na kuseti lingine moja lililofungwa na mchezaji mpya, Juan Iturbe wakati mabao mengine yamefungwa na Maicon na Totti, wakati bao pekee la CSKA limefungwa na Ahmed Musa. Bahati mbaya kwao Roma, Iturbe aliumia kipindi cha kwanza na kutoka. Katika michezo mingine, Athletic Bilbao imelazimishwa safe ya 0-0 na Shakhtar Donetsk wakati Porto iliichapa 6-0 BATE jana.
Gervinho ameng'ara Roma ikiua 5-1 Ligi ya Mabingwa








0 comments:

Post a Comment