Ligi kuu ya nchini Hispania itaendelea tena leo kwa michezo
mingi katika viwanja tofauti huku macho ya mashabiki wengi ni katika
mchezo wa kuhistoria na ushindani mkubwa (El Clasico) kati ya Real
Madrid wakiwa katika uwanja wa nyumbani Santiago Bernabeu
wakiwakalibisha FC Barcelona.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa sababu
utakutanisha wachezaji bora ulimwenguni kama kwa upande wa Real Madrid,
Christiano Ronaldo,James Rodriguez,Toni Kros,Karim Benzema na wengineo
na kwa upande wa timu ya Barcelona kuna wakali kama Lionel
Messi,Neymar,Iniesta na mchezaji Louis Suarez ambaye alikuwa anasubiriwa
kwa hamu sana na mashabiki wake baada ya kuwa anatumikia adhabu yake
aliyokuwa kafungia.Suarez ataonekana kwa mara ya kwanza kesho katika
mchezo huo wa La liga.
Real Madrid itaingia uwanjani huku wakimkosa mshambuliaji wao
mwenye kasi sana Gareth Bale baada ya kuwa na majeraha ya nyama za paja.
0 comments:
Post a Comment