AZAM YATUPWA NJE YA MICHUANO LA SHIRIKISHO..


Wawakilishi wa Tanzania, Azam FC wameng’olewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho.


Azam FC imefungwa mabao 2-0 na wenyeji wake Ferreviario ya Msumbuji maarufu kama Wamakonde katika mechi iliyopigwa leo mjini Beira.
Katika mechi ya kwanza Azam FC ilishinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamzi jijini Dar. Mfungaji akiwa Kipre Tchetche.


Kutokana na kipigo cha leo, maana yake Azam FC imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1 na kuifanya kutoka mapema zaidi katika michuano hiyo ndani ya misimu mitatu.

0 comments:

Post a Comment