LIVERPOOL UBINGWA MKONONI


LIVERPOOL imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Norwich City jioni hii Uwanja wa Carrow Road mjini Norwich, Norfolk, England.
Liverpool ilipata mabao yake kupitia kwa Raheem Sterling dakika ya nne na 62 na Luis Suarez dakika ya 11, wakati mabao ya Norwich yalifungwa na Hooper dakika ya 53 na Snodgrass dakika ya 77.
Liverpool sasa inatimiza pointi 80 baada ya kucheza mechi 35 ikiendelea kuishi kileleni mwa ligi hiyo, mbele ya Chelsea yenye pointi 75 za mechi 35 na Manchester City yenye pointi 71 za mechi 33.
Katika michezo mingine ya ligi hiyo leo, Manchester United imefungwa 2-0 na Everton na Hull City imelala 3-0 mbele ya Arsenal.
Mashujaa: Sterling na Luis Suarez wakishangilia pamoja baada ya kazi nzuri leo.

0 comments:

Post a Comment