SIMBA VS YANGA HAKUNA MBABE-VITUKO VYATAWALA.

Pambano la watani wa jadi limemalizika kwa sare katika mchezo mkali wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa taifa. Simba waliandika bao la kwanza kupitia kwa Haruna Chanongo katika dakika ya 75 kufuatia kazi nzuri ya Uhuru Selemani huku Yanga wakisawazisha katika dakika 86 kupitia Simon Msuva.
Pambano hili lilitawaliwa na vituko ikiwemo Didier Kavumbagu kupewa kadi ya njano baada ya kulichukua taulo la Ivo Mapunda na kwenda kulitupa kwa mashabiki na baadae shabiki wa Yanga kuruka uzio na kulikwapua kwa mara ya pili. Hata hivyo timu zote zilicheza mchezo wa kuvutia na kukosa nafasi nyingi za wazi.

0 comments:

Post a Comment