REAL BINGWA EL CLASICO ,WAIFUNGA BARCA 2-1, BILA RONALDO

REAL Madrid imetwaa Kombe la Mfalme baada ya kuichapa Barcelona mabao 2-1 usiku wa jana katika  Uwanja wa Mestalla mjini Valencia, Hispania.

Real walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 11, mfungaji Angel di Maria akimalizia pasi ya Karim Benzema, lakini Bartra akaisawazishia Barca dakika ya 68 kwa pasi ya Xavi.
Group photo: Real Madrid players pose together after the final as the celebrations begin



Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo akiwa ameshika Kombe la Mfalme usiku wa jana baada ya timu yake, Real Madrid kuifunga Barcelona Uwanja wa Mestalla mjini Valencia katika fainali. Ronaldo hakucheza sababu ya majeruhi.
The boss: Real Madrid coach Carlo Ancelotti is thrown into the air by his players
Shujaa wa Real hii hapo jana alikuwa na nyota wa Wales, Gareth Bale aliyefunga bao la ushindi dakika ya 85 kwa pasi ya Fabio Coentrao.

Wafalme; Mfungaji wa bao la ushindi la Real, Gareth Bale kushoto akishangilia na Alonso kulia



Bingwa Mfalme; Mfungaji wa bao la ushindi la Real, Gareth Bale kulia akipiga shuti pembeni ya Dani Alves

Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alikuwa nje akiendelea kuugulia maumivu yake na aliungana na wenzake kuwapongeza baada ya mechi kwa ushindi huo.
Baada ya kunyakua taji la kwanza msimu huu, Real sasa inaelekeza nguvu zake katika mataji mengine mawili, La Liga na Ligi ya Mabingwa ambako imefika hatua ya Nusu Fainali na itamenyana na mabingwa watetezi, Bayern Munich.
Kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Hispania, Real inachuana na Atletico Madrid walio kileleni na Barca walio nafasi ya tatu.






+12
Mashabiki wa Real Madrid wakisherehekea taji la Copa del Rey Uwanja wa Mestalla




+12
Lionel Messi akilalamika baada ya kipigo cha Barcelona kwa wapinzani wao, Real Madrid mjini Valencia

Ronaldo akitazama mechi  Mestalla





+12Angel di Maria akishangilia baada ya kuifungia bao la kuongoza Real





+12
Bartra akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Barcelona





+12
Gareth Bale akipiga shuti mbele ya Javier Mascherano

CHANZO: BIN ZUBEIRY

0 comments:

Post a Comment