BILA mchezaji bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo, Real Madrid
wanaingia kata EL CLASICO ya 3 na ya mwisho kwa Msimu huu dhidi ya FC
Barcelona usiku wa leo katika uwanja wa Estadio Mestalla Mjini Valencia.
Hii ni fainali ya Fainali ya Kombe la Mfalme, Campeonato de España – Copa de Su Majestad el Rey, kwa kwetu limezoeleka kwa jina la Copa del Rey. Barcelona, ambao wameshatwaa Kombe hili mara 26, mara ya mwisho kulitwaa ni 2012, wakati Real, ambao wamelitwaa mara 18, Mwaka Jana walifungwa katika mechi ya fainali na mahasimu wao Atletico Madrid. Barca na Real zimeshakutana mara mbili Msimu huu kwenye mechi za ligi kuu maarufu kama La Liga, huku Barca wakishinda Mechi zote mbili. Mara ya mwisho kukutana kwenye Copa del Rey ni Mwaka 2011, t
ena
Uwanja huu huu wa safari hii, Estadio Mestalla, ambapo Bao la Dakika za
Majeruhi la Cristiano Ronaldo liliwapa Kombe Real na pia kumpa Kombe la
Kwanza Kocha Jose Mourinho kwenye himaya yake na Real Madrid.
MECHI 3 ZILIZOPITA:
-Real 3 (Benzema 2, Ronaldo) Barcelona 4 (Iniesta, Messi 3), La Liga, Machi 2014
-Barcelona 2 (Neymar, Sanchez) Real 1 (Jese), La Liga, Oktoba 2013
-Real 2 (Benzema, Ramos) Barcelona 1 (Messi), La Liga, Machi 2013
Lakini safari hii kila Klabu ina Meneja mpya, Carlo Ancelotti
na Real na Gerardo Martino kwa Barca, na wanatinga kwenye Fainali hii
wakitokea kwenye matokeo tofauti kabisa.
Barca wanatinga Fainali hii wakiwa kwenye majonzi makubwa kwani
Wiki moja iliyopita walikuwa kwenye ndoto kubwa ya kutwaa Trebo kama
walivyofanya Mwaka 2009 lakini mambo yakapinduka na wakatolewa toka UEFA
na Atletico Madrid na Siku 3 baadae kufungwa 1-0 na Granada kwenye La
Liga na kuachwa wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Atletico na Real huku
Mechi zikiwa zimebaki 5.
Tofauti kabisa, Real wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na
morali ya juu baada ya kufuzu kuingia Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI na pia kuwa kileleni mwa La Liga, pamoja na Atletico, baada ya
kuifumua Almeria 4-0 Siku 3 baadae.
Kila Timu inakabiliwa na Majeruhi wengi huku Barca ikiwa dhoofu
kwenye safu yao ya ulinzi wakiwemo Gerard Pique, Carles Puyol na Marc
Bartra, ambaye kidogo ni nafuu na huenda akacheza, lakini upo uwezekano
mkubwa kwenye Mechi hii Difensi ya Barca ikawa na Viungo, Mascherano na
Busquet, kama Masentahafu wao.
Real wataingia wakiwa na hatihati kuhusu kucheza kwa Staa wao
Cristiano Ronaldo ambae hajacheza Mechi 2 zilizopita akiwa na maumivu.
Carlo Ancelotti ameleeleza jana kuwa Ronaldo hatakuwepo, lakini
kukosekana kwake kunaweza kutoa mwanya kwa ama Asier Illarramendi au
Isco kucheza na kuungana na Angel di Maria, Gareth Bale na Karim Benzema
kwenye mashambulizi.
Ancelotti mapema jana alikaririwa akisema Ronaldo anaweza kucheza kwa sababu anaendelea vizuri, lakini baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi ya leo alithibitisha kuwa nyota huyo atakosekana kabisa. “Cristiano Rinaldo hatakuwepo, lakini tuna wachezaji wengi katika kikosi chetu”. “Tuna imani kubwa na timu hii. Nimekuwa nikijitahidi kukabiliana na majeruhi na nadhani tutafanya kazi nzuri tu”. Aliongeza kocha huyo raia wa Italia ambaye hata hivyo aligoma kutaja kikosi kinachoweza kuanza leo hii. VIKOSI VINATARAJIWA: Real Madrid: Casillas; Carvajal, Ramos, Pepe, Coentrao; Modric, Alonso, Illarra; Di Maria, Benzema, Bale Barcelona: Pinto; Alves, Mascherano, Bartra, Alba; Busquets, Xavi, Iniesta; Neymar, Messi, Sanchez COPA del REY-NJIA YA FAINALI NUSU FAINALI Marudiano [Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2] Jumanne Februari 11 Atletico de Madrid 0 Real Madrid CF 2 [0-5] Jumatano Februari 12 Real Sociedad 1 FC Barcelona 1 [1-3] FAINALI Aprili 16 Real Madrid v Barcelona
0 comments:
Post a Comment