ARSENAL
hapo jana imeichapa mabao 3-1 West Ham Unitede Uwanja wa Emirates jana katika
mchezo wa Ligi Kuu ya England na kufufua matumaini ya kucheza Ligi ya
Mabingwa msimu ujao.
Mabao
ya Gunners jana yamefungwa na Lukas Podolski mawili dakika za 44 na 78
na Olivier Giroud dakika ya 54. Ushindi huo unaifanya Arsenal itimize
pointi 67 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kukamata nafasi ya nne.
Liverpool
ipo kileleni kwa pointi zake 77 za mechi 34, Chelsea ya pili pointi 75
za mechi 34, wakati Manchester City ni ya tatu kwa pointi zake 70 za
mechi 32. 

Kazi nzuri: Lukas Podolski ameifungia mabao mawili Arsenal ikiichapa 3-1 West Ham jana
Kitu nyavuni: Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud amefunga moja jana
0 comments:
Post a Comment