AFRIKA
imetolewa kabisa katika Kombe la Dunia baada ya wawakilishi wake
waliobakia Algeria, kufungwa mabao 2-1 na Ujerumani katika mchezo wa 16
Bora usiku huu Uwanja wa Beira-Rio mjini Porto Alegre.
Ni
hitimisho la siku nyingine mbaya kwa Waafrika, baada ya awali,
wawakilishi wengine waliofika hatua hiyo, Nigeria kutolewa na Ufaransa
kwa mabao 2-0.
Maana
yake, Cameroon, Senegal na Ghana zinabaki kuwa timu zenye mafanikio
zaidi miongoni mwa nchi za Afrika kwenye Kombe la Dunia kwa kuweza
kufika Robo Fainali za michuano hiyo. Simba Wasiofungika walianza 1990
Italia, Simba wa Teranga wakafuatia 2002 Korea na Japan na Nyota Weusi
wakamalizia 2010 Afrika Kusini.
Dakika
90 za mchezo kati ya Ujerumani na Algeria zilimalizika timu hizo zikiwa
hazijafungana, lakini katika 30 za nyongeza mabao ya Andre Schurrle 92
na Mesut Ozil 119 yaliwafuta kabisa Waafrika katika Kombe la Dunia 2014
Brazil, mapema zaidi kuliko fainali zilizopita Afrika Kusini.
Abdelmoumene Djabou aliifungia Algeria bao la kufutia machozi dakika ya mwisho kabisa, Ujerumani ikienda Robo Fainali.
Kikosi
cha Ujerumani kilikuwa; Neuer, Mustafi/Khedira dk70, Mertesacker,
Boateng, Howedes, Lahm, Ozil, Schweinsteiger/Kramer dk109, Kroos,
Gotze/Schurrle dk46 na Muller.
Algeria:
M'Bolhi, Mandi, Belkalem, Halliche/Bougherra dk98, Ghoulam, Lacen,
Mostefa, Feghouli, Soudani/Djabou dk100, Taider/Brahimi dk79 na Slimani.
0 comments:
Post a Comment