NDOTO
za Nigeria kuungana na Cameroon, Senegal na Ghana katika orodha ya timu
za Afrika zilizowahi kucheza Robo Fainali za Kombe la Dunia zimezimwa
leo baada ya kufungwa mabao 2-0 na Ufaransa katika mchezo wa 16 Bora
Uwanja wa Garrincha, Brasilia, Brazil.
Nigeria
iliyotinga 16 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 baada ya kushika
nafasi ya pili Kundi F, ilijitahidi kuwabana Ufaransa kwa muda mrefu,
lakini ‘pumzi iliwakatika’ dakika za mwishoni.
Kabla
ya Paul Pogba kufunga bao la kwanza kichwa dakika ya 79, kipa Vincent
Enyiama alikoswa mabao matatu ya wazi, moja mchomo wa Karim Benzema
ukiondolewa kwenye mstari wa lango na Victor Moses.
Beki
Joseph Yobo naye akajifunga dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya
kutimu dakika 90 za kawaida, katika harakati za kuokoa krosi.
Kikosi
cha Ufaransa kilikuwa: Lloris, Debuchy, Varane, Koscielny, Evra, Pogba,
Cabaye, Matuidi, Valbuena/Sissoko dk90+4, Giroud/Griezmann dk62 na
Benzema.
Nigeria: Enyeama, Ambrose, Yobo, Oshaniwa, Omeruo, Musa, Onazi/Gabriel dk59, Mikel, Moses/Nwofor dk89, Odemwingie na Emenike.
Ulinzi
shirikishi: Paul Pogba akienda hewani mbele ya mabeki wa Super Eagels
kupiga kichwa kuifungia Ufaransa bao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya
Nigeria
0 comments:
Post a Comment