Didier Drogba na Gervinho wameiongoza Ivory Coast kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya El Salvador katika mechi ya mwisho yao ya mwisho ya kirafiki kuelekea Kombe la Dunia huko Brazil.
Tembo hao wa Teranga walianza kuongoza katika dakika ya 9 ya mchezo pale Drogba alipomtengenezea mpira Gervinho ambaye alimalizia kazi.
Vijana hao wa kocha Sabri Lamoshi waliendelea kutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kupata goli la pili kabla ya mapumziko kupitia kwa Drogba.
El Selvador walipata goli lao kupitia mkwaju wa penati uliofungwa na Arturo baada ya Kolo Toure ambaye ametoka kupona Malaria kumkwatua Jonathan Aguilar katika eneo la hatari.
Hiyob ndiyo ilikuwa mechi ya mwisho kwa Ivory Coast ambao watavaana na Japan katika mechi yao ya ufunguzi hapo June 14.
0 comments:
Post a Comment