Nijeria na Kodivaa watafikia raundi ya pili – Mourinho
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho, amesema kuwa Nigeria na Ivory Coast ndiyo mataifa ya Afrika yatakayoweza kufika katika raundi ya pili ya kombe la Dunia la 2014 katika fainali za huko Brazili.
Nigeria ipo katika Kundi D pamoja na Argentina, Irani na Bosnia-Hezegovina, na Mourinho anatarajia kwamba timu ya Nijeria Super Eagles itamaliza mechi za kundi ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Agentina kwa kuwa inakuwa na mchezaji wa Chelsea John Obi Mikel.
“Nitafanya kama nilivyofanya katika Kundi A. Ninasema kuwa Agentina lazima itakuwa mshindi wa Kundi. Kinachonifanya kuamua kuwa Nigeria ina bahati ni kwamba nina mchezaji mmoja pale (John Obi Mikel). Nachukua Nigeria kama mkwezi wa juu,” Mourinho alitangaza kwenye Yahoo's Dirty Tackle.
Kuhusu Ivory Coast inayopatikana katika Kundi C pamoja na Ugiriki, Japani na Colombia, Mourinho alisema kuwa Ivory Coast watakuwa mbele ya Japani na Colombia kwa sababu wana wachezaji kama Didier Drogba aliyefundishwa naye katika Chelsea mnamo 2004-2007.
Nchi tatu nyingine za Afrika kama Cameroon, Ghana na Algeria hazikuweza kutajwa katika utabiri wa Mourinho.
0 comments:
Post a Comment