KOMBE LA DUNIA: ECUADOR WALALA 2-1 NA USWISI MWISHONI!

Switzerland beats Ecuador 2-1 at World CupECUADOR, wakiongozwa na Staa wa Manchester United Antonio Valencia Usiku huu wamelimwaga baada kuongoza Bao 1-0 na kuiruhusu Uswisi kuwafunga 2-1 katika Mechi yao ya Kwanza ya Kundi E la Fainali za Kombe la Dunia kwenye Mechi iliyochezwa huko Estadio Nacional Mjini Brasilia.
Kitu cha kusikitisha mno kwa Ecuador ni kuwa kwenye Dakika ya 92, huku Bango likiwa tayari limeashiria Dakika 3 za Nyongeza, Antonio Valencia alichanja mbuga na kuingia ndani ya Boksi na kumpa Pasi murua Arroyo amalizie tu lakini Mchezaji huyo alifanya mbwembwe na Mpira kunaswa na Behrami na Uswisi kuanza shambulizi lao la nguvu ambalo walifunga Bao lao la ushindi.
Bao hilo lilifungwa na Haris Seferovic kwenye Dakika ya 92 na Sekunde 41.
+++++++++++++++++++
MAGOLI
ECUADOR 1
-Enner Valencia Dakika ya 22
SWITZERLAND 2
-Admir Mehmedi Dakika ya 47
-Haris Seferovic 90 +2:41
+++++++++++++++++++
Mechi zinazofuata kwa Ecuador ni dhidi ya Honduras Ijumaa Juni 20 wakati Uswisi itacheza na France Siku hiyo hiyo.
VIKOSI:
SWITZERLAND: Benaglio, Lichtsteiner, Rodriguez, Von Bergen, Djourou, Inler, Behrami, Shaqiri, Xhaka, Stocker, Drmic.
ECUADOR: Dominguez, Paredes, Ayovi, Guagua, Erazo, Antonio Valencia, Noboa, Gruezo, Montero, Caicedo, E. Valencia.
Refa: Ravshan IRMATOV [Uzbekistan]
KOMBE LA DUNIA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
JUMAPILI, JUNI 15, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Switzerland 2 Ecuador 1
E
Nacional
2200
France v Honduras
E
Estadio Beira-Rio
0100
Argentina v Bosnia
F
Estadio do MaracanĂ£
JUMATATU, JUNI 16, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Germany v Portugal
G
Arena Fonte Nova
2200
Iran v Nigeria
F
Arena da Baixada
0100
Ghana v United States
G
Estadio das Dunas

0 comments:

Post a Comment