PORTO ALEGRE, Brazil, Karim Benzema amekuwa shujaa wa mechi baada ya kufunga magoli mawili katika ya matatu wakati Ufaransa walipoifunga Honduras magoli 3-0.
Ushindi huo umekuwa ahueni kwa Ufaransa ambayo haikufanya vizuri katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Afrika Kusini.

Katika mchezo wa leo Ufaransa ndiyo waliotawala mchezo na kupata goli la kuongoza kwa njia ya mkwaju wa penati iliyofungwa na Benzema baada ya Wilson Palacios wa Honduras kumchezea madhambi Paul Pogba ndani ya kumi na nane.
Benzema alisababisha goli la pili tena katika dakika ya 48 baada ya kipa wa Honduras kujifunga akijaribu kuokoa shuti lake, goli ambalo lilileta utata na kuamuliwa na teknolojia mpya ya Goal line.Dakika ya 72 alikuwa ni Benzema tena aliyefunga goli la tatu kwa Ufaransa akipiga shuti kali kumalizia shuti la Mathieu lililotemwa na kipa.
Akizungumza baada ya mchezo huo Benzema alisema hii ni mara yake ya kwanza kushiriki kombe la dunia na ameridhishwa na matokeo, akiongeza kuwa ilikuwa ni muhimu kushinda katika mechi hiyo.
Katika mchezo wa leo Ufaransa waliwatawala kikamilifu Honduras ambapo kipa wa Ufaransa hakugusa mpira tangu dakika ya 31 hadi mwisho wa mchezo.
Honduras walimaliza wakiwa 10 baada ya mchezaji wao Palacios kutolewa kwa kadi nyekundu kutokana na madhambi aliyomchezea Paul Pogba.

0 comments:
Post a Comment