UJERUMANI YAIFUMUA URENO 4-0 NA RONALDO WAO, MULLER APIGA HAT TRICK, PEPE ALIMWA NYEKUNDU

MAJANGA! Ureno ikiongozwa na Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo imechapwa mabao 4-0 na Ujerumani jioni ya leo katika mchezo wa Kundi G Kombe la Dunia, Uwanja wa Fonte Nova mjini Salvador Bahia, Brazil.
Kiboko ya Wareno leo alikuwa ni mshambuliaji Thomas Muller aliyefunga mabao matatu peke yake, dakika za 12 penalti baada ya Mario Gotze kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari, 45 na 88, wakati bao lingine lilifungwa na Mats Hummels dakika ya 32 baada ya kazi nzuri ya Tony Kroos.
Beki wa Ureno, Pepe alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 37 na refa Milorad Mazic wa Serbia, baada ya kumpiga kichwa Muller kwa hasira kufuatia mshambuliaji huyo wa Ujerumani kujiangusha wakati wakikabiliana.
Kikosi cha Ujerumani kilikuwa; Neuer, Boateng, Mertesacker, Hummels/Mustafi dk73, Howedes, Lahm, Khedira, Kroos, Ozil/Schurrle dk62, Muller na Gotze.
Ureno: Rui Patricio, Joao Pereira, Pepe, Bruno Alves, Fabio Coentrao/Andre Almeida dk65, Veloso/Ricardo Costa dk46, Joao Moutinho, Meireles, Nani, Almeida na Ronaldo. 
Ushindi wa aina yake: Wachezaji wa Ujerumani wakimpongeza Thomas Muller (kushoto) baada ya kukamilisha hat trick dhidi ya Ureno

0 comments:

Post a Comment