AZAM
FC imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa
nchi za Maziwa Makuu, maarufu kama Rollingston baada ya kuichapa timu ya
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ya Mgulani Twalipo bao 2-0 katika
fainali jioni hii Uwanja wa karume, Dar es Salaam. Jamil Mchaulu
‘Balotelli’ aliyefunga bao la kwanza dakika ya tatu, baada ya kuwatoka
vizuri beki wa kulia wa Twalipo, Ally Mbonde na beki wa kati Ally
Athumani kisha kumtungua kipa wao, Kulwa Baumba.
Huku Adam Omar Soba akiifungia Azam FC bao la pili dakika ya 88 na kuihakikishia ushindi wake.
|
0 comments:
Post a Comment