KOCHA
Louis van Gaal ameendeleza wimbi la ushindi baada ya Manchester United
kuifunga kwa penalti 5-3 Inter Milan kufuatia safe ya 0-0 katika mchezo
wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa FedEx Field mjini Washington, penalti za United zilitiwa nyavuni na Ashley Young, Javier Hernandez, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Darren Fletcher wakati Marco Andreolli wa Inter aligongesha mwamba. Van Gaal akipanga vikosi viwili, kimoja kila kipindi.
Man United kipindi cha kwanza: Lindegaard, Smalling, Jones, Evans, Valencia, Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney, Welbeck
Kipindi cha pili: De Gea; M Keane, Evans, Blackett; Young, Cleverley, Fletcher, Kagawa, Shaw; Zaha, Nani/Hernandez dk77.
Inter
Milan: Handanovic/Carrizo dk63, Ranocchia, Vidic/Andreolli dk72, Juan
Jesus, D'Ambrosio, Jonathan, Kuzmanovic/Laxalt dk63, Krhin/M'Vila dk46,
Dodo/Nagatomo dk63, Botta/Taider dk63 na Icardi.
0 comments:
Post a Comment