BRAZIL BWANA! -YAKOSA USHINDI WA TATU, YAPIGWA TATU NA UHOLANZI.

WENYEJI Brazil wamemaliza Fainali za Kombe la Dunia kwa huzuni na fedheha kubwa baada ya kuikosa hata Nafasi ya Tatu walipotandikwa Bao 3-0 na Netherlands huko Mjini Brasilia na kuwafanya Mashabiki wao wawazomee mwishoni mwa Mechi. Lakini Brazil waliingia Uwanjani kwa kushangiliwa na hasa Neymar, ambae ni Majeruhi, kuingia huku akiwa amevaa Jezi na kupokewa kwa shangwe kubwa.

Wakichezesha Kikosi kilichobadilisha Wachezaji 6 toka kile kilichobamizwa 7-1 kwenye Nusu Fainali na Germany, Brazil, kwa mara nyingine tena walionyesha udhaifu mkubwa wa Difensi yao ambao ulitoa zawadi ya ushindi kwa Netherlands.
Netherlands, ambao kwenye Mechi zao za Robo Fainali na Nusu Fainali walishindwa kufunga hata Bao moja baada zote kwisha 0-0 na kuamuliwa kwa Mikwaju ya Penati, walipata Bao lao la Kwanza Dakika ya Tatu tu kupitia Penati ya Robin van Persie.
Penati hiyo ilitoka kwa Nahodha wao Thiago Silva, ambae ndio kwanza ametoka Kifungo cha Mechi moja, alipomvuta Arjen Robben na kunusurika kupewa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 16, David Luiz nae akatoa ‘boko’ jingine kwa kupiga Kichwa kibovu cha kuokoa na Mpira kutua kwa Daley Blind aliefunga Bao la Pili.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO:
-Hii ni mara ya kwanza tangu 1940 kwa Brazil kufungwa Mechi 2 mfululizo Nyumbani kwao. Mwaka 1940, walifungwa 3-0 na Argentina na kisha 4-3 na Uruguay.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Bao la Tatu la Netherlands lilifungwa katika Dakika za Majeruhi na Wijnaldum na kuwapa Netherlands ushindi wa 3-0 na kukamata Nafasi ya Tatu.
Leo Usiku, Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2014 zinakamilika kwa Mechi ya Fainali kati ya Argentina na Germany.
VIKOSI:
Brazil:
12 Julio César
23 Maicon
14 Maxwell
17 Luiz Gustavo (Fernandinho - 45')
03 Thiago Silva
04 David Luiz
16 Ramires (Hulk - 73')
08 Paulinho (Hernanes - 57')
21 Jo
19 Willian
11 Oscar
Netherlands:
01 Cillessen (Vorm - 93')
15 Kuyt
05 Blind (Janmaat - 70')
04 Martins Indi
02 Vlaar
03 de Vrij
16 Clasie (Veltman - 90')
08 de Guzmán
20 Wijnaldum
09 van Persie
11 Robben
REFA: Djamel Haimoudi [Algeria]

0 comments:

Post a Comment