FAINALI KOBE LADUNIA: YAFAHAMU MAPUNGUFU YAARGENTINA NA UJERUMANI HAPA.

Baada ya safari ndefu ya Mwezi mzima iliyoanzia Juni 12, hapo Jumapili Fainali za Kombe la Dunia Nchini Brazil zitafikia tamati huko Estadio Maracana, Jijini Rio de Janeiro Nchini Brazil, kwa Mechi ya Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Germany na Argentina.
Huu ni Mtanange kati ya La Albiceleste, kama inavyoitwa Argentina ikimaanisha Nyeupe na Bluu, Rangi ya Bendera ya Nchi yao, dhidi ya Die Mannschaft, ikimaanisha Timu kama inavyoitwa Germany.
Germany imetinga Fainali hii kwa kishindo kikubwa kilichotikisa Dunia baada ya kuwabwaga Wenyeji wa Mashindano Brazil Jumanne iliyopita kwa kipondo cha Bao 7-1 huku wakifunga Bao zao 5 za kwanza ndani ya Dakika 29 na Bao lao la Pili hadi la 5 yakipigwa ndani ya kipindi cha Dakika 6 tu.
Argentina walipata msukosuko kwenye Nusu Fainali yao na Netherlands kwa kwenda Dakika 120 wakiwa Sare 0-0 na hatimae kufuzu kwa Mikwaju ya Penati 4-2 hapo Jumatano.
Fainali hii ya Jumapili inakumbushia Fainali za Miaka ya 1986 na 1990 miamba hii ilipopambana.
Fainali hizo ndizo mara ya mwisho kwa Nchi hizo kutwaa Kombe la Dunia wakati Argentina ilipoifunga West Germany huko Mexico Mwaka 1986 na Germany kuifunga Argentina Mwaka 1990 na kuwa Mabingwa wa Dunia.
Tangu wakati huo, Argentina na Germany hazijatwaa tena Kombe la Dunia.
Kwenye Mechi za hivi karibuni kwenye Kombe la Dunia kati ya Argentina na Germany, Kikosi cha Joachim Loew ndio kimekuwa kidedea kwa kuishinda Argentina kwa Penati Mwaka 2006 kwenye Mashindano yaliyochezwa Nchini Germany na huko Afrika Kusini Mwaka 2010, Germany iliibamiza Argentina 4-0.
Ikiwa Germany itaishinda Argentina hiyo Jumapili, hii itakuwa mara ya kwanza kwa Nchi ya Ulaya kutwaa Ubingwa Bara la Marekani ya Kusini.
BRAZIL-SAFARI YA FAINALI:
ARGENTINA
HATUA
GERMANY
v Bosnia 2-1
KUNDI
v Portugal 4-0
v Iran 1-0
KUNDI
v Ghana 2-2
v Nigeria 3-2
KUNDI
v USA 1-0
v Switzerland 1-0
RAUNDI YA PILI
v Algeria 2-1
v Belgium 1-0
ROBO FAINALI
v France 1-0
v Netherlands 0-0 [Penati 4-2]
NUSU FAINALI
v Brazil 7-1

TATHMINI:
Bila shaka, baada ya kuibamiza Brazil Bao 7-1, Germany wataingia kwenye Fainali hii wakiwa kifua mbele kwa kujiamini.
Staili ya Germany ni lile Soka ambalo limetulia lenye pasi rahisi si zile nyingi kama Tiki-Taka ya Spain lakini upenyo ukipatikana tu ni wepesi wa kufanya shambulizi la nguvu na kustukiza.
Kocha wa Germany, Joachim Loew, alibadilisha mbinu na mfumo huko Brazil kwa kuamua kumrudisha Nahodha wake Philipp Lahm kwenye nafasi yake ya asili ya Fulbeki wa Kulia kutoka Kiungo Mkabaji na kwenye Kiungo kuweka Mtu 3, Toni Kroos, Bastian Schweinsteiger na Sami Khedira
Kwa upande wa Argentina, ukimwondoa Lionel Messi, mara nyingi Wachezaji wao wengine hawaonyeshi kuwa tishio.
Tangu mwanzoni mwa Mashindano haya, Messi amekuwa akiibeba Timu kwa ama kufunga Bao zao muhimu au kuchangia katika kufunga Bao zao za ushindi.
Ukimwondoa Angel di Maria, ambae kidogo alionyesha uhai lakini akaumia na pengine hatacheza Fainali hii, wanao Ezequiel Lavezzi na Gonzalo Higuain ambao ufungaji wao umekuwa adimu au hamna kabisa.
Licha ya ile imani ya Wachambuzi wengi kwamba Difensi ya Argentina ni ‘nyanya’, Nchi hiyo imeonyesha umahiri mkubwa kwa kuweza kucheza Mechi 4 bila kufungwa hata Bao.
Difensi yao ya Mtu 4, Zabaleta, Demichelis, Garay na Rojo, imekuwa ikilindwa vilivyo na Kiungo Mkabaji Javier Mascherano ambae ameibuka kuwa mmoja wa Nyota waliong’ara mno huko Brazil kwa mchango wake mkubwa.
Kocha wa Argentina, Alejandro Sabella, atakuwa akisali kuomba Difensi yake iweze kuhimili vishindo vya ‘Mashine ya Kijerumani’ huku akiomba sana Messi ang’are japo kwa sekunde moja tu ili awape Bao la ushindi.
DONDOO MUHIMU:
Uso kwa Uso
Argentina-Ushindi 9
Germany-Ushindi 6
Wafungaji wao Bora huko Brazil
Germany: Thomas Muller (5)
Argentina: Lionel Messi (4)
Takwimu
-Huko Brazil, Argentina imefunga Bao 8 wakati Germany ina Bao 17.
-Germany sasa wameipiku Brazil na kuwa ndio Wafungaji Bora Fainali za Kombe la Dunia wakiwa na Mabao 223.

REFA: Nicola Rizzoli [Italy]
+++++++++++++++++++++++++++++++
Kumbukumbu
Argentina 3 West Germany 2, Fainali Kombe la Dunia, Mexico 1986
Fainali za Mwaka huo zitakumbukwa kwa ajili ya Maradona wakati Germany ilipotanguliwa Bao 2-0 mapema Kipindi cha Pili.
Germany, wakiongozwa na Franz Beckenbauer, wakajitutumua na kufanya Gemu iwe 2-2 kwa Bao za Karl-Heinz Rummennigge na Rudi Voller huku Dakika zikibaki 10.
Huku kila Mtu akitegemea Mechi inaenda Dakika za Nyongeza 30, Maradona akatoa pande safi kwa Jorge Burruchaga aliekutana uso kwa uso na Kipa Schumacher na kupiga shuti lililompita Kipa huyo na kuipa Argentina ushindi wa Bao 3-2.
Hicho kilikuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Germany kwenye Fainali ya Kombe la Dunia na ndio mara ya mwisho kwa Argentina kuwa Bingwa wa Dunia.
Argentina 0 West Germany 1, Fainali Kombe la Dunia, Italy 1990
Argentina na Germany zilikutana tena Fainali iliyoufuata huko Stadio Olympico Jijini Rome na Germany kulipa kisasi.
Mechi hiyo ilishuhudia Mchezaji wa Argentina Pedro Monzón akitolewa kwa Kadi Nyekundu na kuweka Rekodi ya kuwa Mtu wa kwanza kutolewa nje kwenye Fainali.
Bao la ushindi la Germany lilipatikana kwa Penati iliyotolewa kwa faulo dhidi ya Rudi Voller na Andreas Brehme kufunga Penati hiyo.
KOMBE LA DUNIA
RATIBA
**Saa za Bongo
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014
SAAMECHIKUNDIUWANJA 2200Germany v ArgentinaFAINALIEstadio do Maracanã, Rio de Janeiro
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014
SAAMECHIKUNDIUWANJA
2200Germany v ArgentinaFAINALIEstadio do Maracanã, Rio de Janeiro

0 comments:

Post a Comment