Na Boniface Wambura, Johannesburg
Kikosi
cha Taifa Stars kimewasili salama juzi (Julai 30 mwaka huu) hapa Johannesburg
kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya
mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo-
asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho
yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya baadaye jioni kuanza
safari ya Maputo.
Wakati
huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni
atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia
wachezaji.
0 comments:
Post a Comment