HII ni Mechi ambayo kila upande, baada kuhuzunishwa na kushindwa kutinga Fainali, hautaki kucheza lakini hulazimika kucheza ili mradi kukamilisha Ratiba tu.
Kocha wa Netherlands, Louis van Gaal, ambae Timu yake ilibwagwa kwenye Nusu Fainali na Argentina kwa Mikwaju ya Penati 4-2, ameshasema kuwa si haki kwa Timu kucheza Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu wa Kombe la Dunia wakati kila mmoja alikuja kubeba Kombe la Dunia.
Lakini kwa Wenyeji Brazil inaelekeo lengo lao ni tofauti kabisa hasa baada ya kufedheheshwa Nyumbani kwao kwa kushindwa kuingia Fainali na kutwaa Kombe la Dunia lakini pia hilo limetokea baada ya kuaibishwa mno walipotwangwa Bao 7-1 na Germany kwenye Nusu Fainali.
Baada ya maafa hayo, kila Mtu kwenye Kambi ya Brazil ametaka wajifariji japo kidogo kwa kuifunga Netherlands na angalau kushika nafasi ya Tatu.
Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari, ameshasema wao watacheza kulinda hadhi ya Jezi ya Timu ya Taifa.
Staa wao mkubwa, Neymar, ambae alivunjwa Mfupa wa mdogo wa Mgongoni kwenye Mechi ya Robo Fainali na Colombia na hivyo kushindwa kucheza Mechi na Germany na kuondolewa Kambini, amerudi Kambini mwa Brazil ili kuwahamasisha wenzake kwa ajili ya Mechi na Netherlands.
Neymar amesema: “Tulipata nafasi ya kuwa Mabingwa Nchini kwetu na tukashindwa. Hatukuonyesha jinsi Soka la Brazil lilivyokuwa zuri, la juu na kuvutia lakini lazima tuitazame Mechi hii ya mwisho kama Fainali. Ushindi hautafuta uchungu tunaosikia hii Leo lakini ni muhimu.”
Ingawa Neymar hataweza kucheza lakini Brazil watamkaribisha tena Nahodha wao Thiago Silva ambae hakucheza Mechi na Germany alipokuwa akitumikia Kifungo cha Mechi moja baada kuzoa Kadi za Njano mbili.
Uso kwa Uso:
Mechi: 11
Brazil: Ushindi 3
Netherlands: Ushindi 3
Sare: 5
VIKOSI VINATARAJIWA:
Brazil: Cesar, Marcelo, Silva, Alves, Luiz, Gustavo, Fernandinho, Hulk, Oscar, Fred, Willian
Netherlands: Cillessen; Indi, Vlaar, Vrij; Blind, Wijnaldum, Guzman, Kuyt; Sneijder; Robben, Van Persie.
REFA: Djamel Haimoudi [Algeria]
KOMBE LA DUNIA
RATIBA
**Saa za Bongo
MSHINDI WA TATU JUMAMOSI, JULAI 12, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Brazil v Netherlands |
MSHINDI WA 3 |
Nacional, Brasilia |
FAINALI JUMAPILI, JULAI 13, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2200 |
Germany v Argentina |
FAINALI |
Estadio do MaracanĂ£, Rio de Janeiro |
0 comments:
Post a Comment