Liverpool imethibitisha kwamba wamekubali kumuuza Straika wao Luis Suarez.
kwa Barcelona.
Wiki ijayo Suarez atasafiri kwenda Barcelona kupimwa Afya yake na kusaini Mkataba wa Miaka Mitano.
Hivi sasa Suarez yupo kwenye Kifungo cha Miezi Minne alichopewa na
FIFA baada kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini wakati wa Mechi
ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil hapo Juni 26.
Tanga mwanzoni mwa Msimu uliopita Suarez amekuwa akitaka kuihama
Liverpool na Mwaka Jana bado kidogo ahamie Arsenal ambao walitoa Ofa ya
Pauni Milioni 40 na Pauni Moja juu ili kumnunua lakini walikataliwa.
Baada ya hapo Suarez akasaini Mkataba mpya wa muda mrefu na Liverpool
na kuifungia Bao 30 kwenye Ligi Kuu England na kuibuka Mchezaji Bora wa
Mwaka baada kuteuliwa na PFA, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa huko
England, na FWA, Chama cha Wanahabari wa Soka, pia cha England.
Inaaminika Barcelona wameafiki kulipa Dau la Pauni Milioni 75 ambalo
ndio lipo kwenye Kipengele cha Mkataba wa Suarez na Liverpool ikiwa
atataka kuhama kabla Mkataba wake kumalizika.
Ikithibitisha kuhama kwa Suarez, taarifa ya Liverpool ilisema:
“Liverpool FC inathibitisha Luis Suarez ataondoka Klabuni baada kufikia
makubaliano ya Uhamisho na FC Barcelona. Mchezaji sasa yupo huru
kukamilisha taratibu za Uhamisho.”
Kwa upande wake, Suarez alitoa shukrani kwa Klabu na Mashabiki wake ambao amewataka kuelewa uamuzi wake.
0 comments:
Post a Comment