Lionel Messi na Argentina wamepiga hatua muhimu kuelekea fainali za kombe la dunia baada ya kuwatoa Ubelgiji kwa bao 1-0.
Bao pekee la Argentina na mchezo wa leo limefungwa na Gonzalo Higuain katika dak. ya 8, baada ya kupata msaada mkubwa kutoka kwa Messi ambaye alifanya mpango kutoka kati kati na baadae kutoa pasi safi kwa Higuain ambaye alimaliza kwa shuti kali la kariu na nje ya 18.
Baada ya ushindi huo, Argentina wameongeza tishio lao kuelekea fainali ya kombe la dunia.Ubelgiji kwa upande wao watapaswa kujilaumu kwa nafasi nyingi walizozikosa ya muhimu ikiwa ni ile ya Lukaku ambaye alishindwa kumalizia mpira ndani ya dakika za nyongeza alipokuwa katika 18.
0 comments:
Post a Comment