UBELGIJI YAIPANDISHA NDEGE U.S-YAICHAPA 2-1

Romelu Lukaku kulia akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Ubelgiji bao la pili katika ushindi wa 2-1

Romelu Lukaku amegeuka shujaa wa ubelgiji baada ya kuifungia timu yake  bao la pili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Marekani mchezo wa mwisho wa 16 Bora Kombe la Dunia nchini Brazil usiku huu. Lukaku pia alimtengenezea Kevin de Bruyne kufunga bao la kwanza, wakati bao pekee la Marekani lilifungwa na Julian Green katika mcbezo huo uliodumu kwa dakika 120, baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. Jumatano ni mapumziko na Robo Fainali zitaanza kuchezwa Alhamisi.

0 comments:

Post a Comment